Mrimbwende
Zawadi Dotto (Pichani) ameibuka kidedea katika Mashindano ya Miss
Albinism Kanda ya Ziwa yaliyofanyika usiku wa Kuamkia leo Jijini Mwanza.
Miss
Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshiki katika
Mashindano hayo ambayo ni maalumu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa
ngozi kwa ajili kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya urimbwene hii
ikiwa pia ni ishara ya kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza
kushiriki katika shughuli na mashindano mbalimbali.
Mashindano
hayo yanaandaliwa na Taasisi ya kusaidia Watu wanaoishi katika
Mazingira hatarishi iitwayo SAVE VUNERABLE FOUNDATION ya Jijini Dar es
Salaam.
Mratibu
wa Shirika hilo Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha kwamba, baada ya
mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini, Washindi wa Kanda hizo
watashindanishwa Jijini Dar es salaam ili kumpata Mshindi wa Kitaifa wa
MISS ALBINISM 2016.
Wshiriki
Saba wa Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa na umri wao katika mabano
ambapo kutoka Kushoto ni Hajra Sadru (22), Antonia Mathias William (17),
Furaha Edward John (17), Pendo Faustine (15), Zabibu Abdallah (18),
Zawadi Dotto (17) pamoja na Asteria Christopher.
Washiriki walioingia Nne bora ambapo kutoka kushoto Hajra Sadru, Furaha Edward, Zabibu Abdallah na Zawadi Dotto
Baada
ya Mtifuano mkali hatimae majaji wakatangaza washini. Furaha Edward
mshindi wa tatu (Kushoto), Hajru Sadru mshindi wa pili (katikati) na
Zawadi Dotto akaibuka kuwa mshindi wa Kwanza (aliepiga magoti).
Mshindi
wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni
Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi.
Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.
Mshindi
wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni
Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi.
Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.
Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Kulia Mshindi wa Pili na Kushoto Mshindi wa Tatu
Kampuni
ya Visimbuzi (Ving'amuzi) ya StarTimes ilikuwa miongoni mwa makampuni
yaliyosaidia kufanikisha mashindano hayo. Mwenye Kinasa sauti ni Erick
Makonya ambae ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa akitaja
zawadi zilizotolewa kwa washindi na Kampuni hiyo ambapo Mshindi wa
Kwanza amejinyakulia Simu ya StarTimes aina ya Solar5, Mshindi wa Pili
simu aina ya P40 StarTimes na Mshindi wa tatu amejishindia simu aina ya
B27 zote zikiwa ni android kutoka StarTimes.
Baadhi
ya Wageni waalikwa wakiongozwa na Marcella Mayala ambae ni Katibu
Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, wakiwa
katika picha ya Pamoja na washindi.
Alexander Exaud Mutowo ambae ni Mratibu wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION
lililoandaa mashindano hayo akizungumza wakati wa mashindano hayo,
ambapo amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia utatuzi wa
changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwemo
kuunga mkono juhudi za shirika hilo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa
jiko katika katika kituo cha kuwahifadhi watu wenye ulemavu wa ngozi
Buhangija kilichopo Mkoani Shinyanga.
Fredy Samwel Kaula ambae ni Mwenyekiti wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION akizungumza katika Mashindano hayo
Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS akizungumza wakati wa mashindano hayo
Mwenye
kinasa sauti ni Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya
Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, akifungua mashindano
hayo.
Amesema ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza itaendeleza ushirikiano na Shirika la VUNERABLE FOUNDATION kwa ajili ya kupata wadau wa kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi.
Dickson
Kiringo a.k.a Mr.White ambae ni Msanii chipukizi wa Muziki wa Kizazi
kipya akitoa burudani. Msanii Barnaba Boy aliahidi kumsaidia Mr.White
ili arekodi nyimbo mbili katika studio yake ikiwa ni bure kabisa.
Msanii Barnaba Boy akitoa burudani katika shindano la Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.
Majaji ambapo kutoka Kushoto ni Jaji Angelina Chuma, Jaji Mkuu Jalia Mtani na Jaji Lilian Lambo
Wa
pili kulia ni Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism
Sociaty TAS pamoja na wadu wengine wakifuatilia mashindano hayo
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa BINAGI MEDIA GROUP
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269