Breaking News

Your Ad Spot

Feb 11, 2016

WAISLAMU 200 WA NIGERIA WAPANDISHWA KIZIMBANI

Waislamu 200 wa Nigeria wapandishwa kizimbani
Wanaharakati wapatao 200 wa Kiislamu waliokamatwa katika operesheni ya kikatili ya jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka jana wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumiliki silaha kinyume cha sheria na kuvuruga amani.
Kesi hiyo ilisikizwa hapo jana ndani ya gereza kuu la eneo la Kaduna, kaskazini mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika, ambako wamezuiliwa tangu mwezi Disemba katika mazingira magumu.
Hussein Ibrahim, wakili wa wanaharakati hao amesema kuwa, wateja wake ghairi ya vijana wanne wenye umri wa chini ya miaka 18 watasalia kizuizini hadi kesi hiyo itakaposikizwa tena mnamo Machi 29.(VICTOR)
Itakumbukwa kuwa, Tarehe 12 hadi 14 Disemba mwaka uliopita wa 2015, jeshi la Nigeria lilishambulia kituo cha kidini na nyumba ya kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky katika mji wa Zaria na kuua mamia ya Waislamu wasio na hatia. Hatima ya Sheikh Zakzaky ambaye alipigwa risasi kadhaa katika hujuma hiyo, bado haijajulikana mpaka sasa.
Siku chache zilizopita, wanaharakati wa Nigeria walifichua kuwa wamegundua kaburi la umati la Waislamu katika makaburi ya Mando Kaduna na kusema kuwa, kaburi hilo ni moja ya makaburi ya umati ambamo jeshi la Nigeria lilizika zaidi ya maiti elfu moja za Waislamu wa mji wa Zaria.CHANZO:IRAN SWAHILI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages