Breaking News

Your Ad Spot

Feb 3, 2016

VIONGOZI WA NGAZI YA VIJIJI WATAKIWA KUSHIRIKI KATIKA KUTOKOMEZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU HADI KUFIKIA MACHI 30 MWAKA HUU

1Waziri wa afya,maendeleo ya Jamii,jinsia,wazee na watoto,ummy mwalimu akiongea na kikosi kazi cha udhibiti wa ugonjwa wa kipindupindu,kulia nina kaimu mganga mkuu wa mkoa wa dodoma,dkt.nassoro mzee.
2Kaimu mganga mkuu mkoa wa dodoma dkt.nassoro mzee akisoma taarifa ya hali ya kipindupindu ya mkoa
3
4Baadhi ya kikosi hicho toka idara na wadau mbalimbali wakimsikiliza waziri huyo.
5Kaimu mganga mkuu wilaya ya bahi dkt. Gerald Maro akielezea jambo ,kikosi kazi toka wizara ya afya na wale wa mkoa(hawapo pichani) mara baada ya kufika kwenye kambi ya kipindupindu iliyopo kwenye zahanati ya isangha iliyopo wilayani bahi, Kulia ni bwana afya wilaya ya bahi selemani yondu
6Mtaalamu toka wizarani dkt. Vida Makundi(wakwanza kushoto)akifafanua jambo kwenye kambi hiyo
7Mwenyekiti wa kijiji cha Isangha,Andrea Lusinde(katikati) akielezea jinsi kijiji hicho kilivyoweza kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na kipindupindu pamoja na ujenzi wa vyoo na kuvitumia,jumla ya vyoo zaidi ya 300 vimejengwa katika kaya,kulia ni diwani wa kata ya chibelela mh.chalula Gerald.
………………………………………………………………………
Na.Catherine Sungura_Dodoma
Viongozi wote kuanzia ngazi ya vijiji wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu hadi kufikia tarehe 30 machi mwaka huu
Wito huo umetolewa leo na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Ummy Mwalimu wakati alipokutana na kikosi kazi cha cha udhibiti wa kipindupindu Mkoa wa Dodoma
“Kipindupindu siyo suala ya afya peke yake,bali ni suala mtambuka hivyo sekta zote zinapaswa kujumuika katika kupambana na kutokomezwa ugonjwa Huu
Ummy alisema kipindupindu bado ni changamoto na nina janga hivyo kila mikoa inatakiwa kuliwekea kipaumbele kwakuwa ugonjwa huo unaua kwa haraka hivyo viongozi wote washiriki kikamilifu na si kuwaachia waganga.wakuu wa mikoa au wilaya
Aidha alisema licha ya kuwa na sheria ndogo Za kila halmashauri za kusimamia usafi na mazingira lakini katika kudhibiti kuenea kwa kipindupindu lazima liatakuja suala la kufungia biashara hususan za mbogamboga,matunda pamoja na chakula”suala la kukusanya mapato lipo na litaendelea kuwepo lakini suala la kipindupindu linapoteza maisha,maisha hayatafutwi lakini pesa zinatafutwa lakini ukikosea utapoteza maisha ya watu wengi”
Ummy alisema tangu kipindupindu kiingie nchini agosti mwaka jana,halmashauri zimetumia pesa nyingi katika kutokomeza ugonjwa huo,lakini wangeweza kuzuia mapema,pesa hizo.zingeenda kutatua tatizo la madawati katika shule za msingi nchini
“Mnapoona hamjaridhika na uendeshaji wa migahawa,msisite kuzifungia mara moja,mapato mtakusanya haraka kwa kuwa na nguvu za pamoja baada ya kutokomeza ugonjwa na kuweza kuingiza mapato mengi na kwa haraka tofauti na kuwa na hilo tatizo Hatahivyo alizitaka vikosi vyote vya mikoa nchi,kuwashirikisha wadau wote wakiwemo viongozi wa dini zote kuweza kuelimisha kuweza kutoa elimu ya jinsi gani ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kwa waumini wao
Mkoa wa dodoma umetumia takribani shilingi milioni 124 za kitanzania toka kipindupindu,hadi leo kuna wagonjwa wanne katika kambi ya kipindupindu wilaya ya bahi,jumla ya wagonjwa 450 waliugua na vifo12,wilaya zilizoathirika ni bahi,dodoma mjini na chamwino

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages