Breaking News

Your Ad Spot

Feb 11, 2016

UMOJA WA MATAIFA WAONYA KWAMBA WASICHANA WENGI HATARINI KUFANYIWA UKEKETAJI


Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki- Moon.
Umoja wa mataifa umeonya kwamba mamilioni ya wasichana wako hatarini kufanyiwa ukeketaji.
Zoezi hilo ambalo linafanyika kwa kukata baadhi ya sehemu za siri za mwanamke halina faida yoyote ya kiafya na inaweza kusababisha kutoka damu kwa kiasi kikubwa , maambukizo, maumivu na baadaye matatatizo katika uzazi.
Baadhi ya wanawake wanafariki dunia kutokana na kitendo hicho.
Wakili mmoja wa Colombia na mwanaharakati anayepinga zoezi la ukeketaji Patricia Tobon anasema amepoteza mama zake wadogo watatu kutokana na kitendo hiki anasema “nilipokuwa na miaka 9 mama yangu aliniambia dada zake watatu wamefariki dunia kwasababu bibi aliwafanyia ukeketaji. Lakini mama yake aliwaokoa yeye na dada yake kutoka kwenye tabia hii.(VICTOR)
Tobon anatoka kabila la Embera kabila pekee huko Amerika kusini ambalo linafanya ukeketaji wa wasichana.
Tabia hii pia inafanyika katika sehemu kubwa ya bara la Afrika , mashariki ya kati na Asia .Shirika la Umoja wa mataifa la idadi ya watu ambalo linafanya kazi kuelimisha watu kuhusu hatari za ukeketaji linaeleza zaidi ya wasichana milioni 125 walio hai hii leo wamepitia ukeketaji katika nchi 29.
Mwimbaji wa Mali na mwanaharakati Inna Modja alipitia ukeketaji akiwa na umri mdogo wa miaka 4. Anasema alipata maumivu ya mwili na kisaikolojia “nilijiona sitaweza tena kuwa mwanamke kwasababu kuna kitu nakosa.CHANZO:RFI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages