TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA
WA KIPINDUPINDU NCHINI PAMOJA NA TAHADHARI YA UGONJWA WA HOMA YA ZIKA,
LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO Y
A JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 8 FEBRUARI 2016.
A JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 8 FEBRUARI 2016.
…………………………………………………………………………………………..
Kuhusu ugonjwa wa kipindupindu,
huu ni mwendelezo wa taarifa ya wiki kwa umma, ya mwenendo wa ugonjwa
huu hapa nchini. Hadi kufikia tarehe 7 Februari 2016, jumla ya watu
15325 wameugua ugonjwa huo, na kati yao watu 238 wamepoteza maisha kwa
ugonjwa huu.
Takwimu za Kuanzia tarehe 1 hadi 7
Februari 2016, zinaonyesha kuwa idadi ya wagonjwa walioripotiwa wiki
hii imepungua kutoka 459 ya wiki iliyoishia tarehe 31 Januari hadi 258
ambapo ni sawa na punguzo la asilimia 44. Kuna vifo 5, sawa na idadi ya
vifo vilivyoripotiwa katika wiki iliyopita.
Jumla ya mikoa ambayo imeripoti
kuwa na wagonjwa ni 13 ambapo mkoa wa Mara ndio umeongoza kwa kuripoti
idadi kubwa zaidi ya wagonjwa ukilinganishwa na mikoa mingine, ukiwa na
wagonjwa 73 (Musoma Vijijini 33, Musoma mjini 5, Bunda 1, Butiama 13,
na Tarime Vijijini 21), ukifuatiwa na mkoa wa Mwanza (70)- (Ukerewe 21,
Nyamagana 24, Ilemela 8, Sengerema 5 na Buchosa 12). Mikoa mingine ni
pamoja na Simiyu (30), Morogoro (26) na Kilimanjaro (16).
Katika mapambano ya kudhibiti
mlipuko huu wa Kipindupindu, kuna changamoto mbalimbali zilizobainishwa
na Wizara yangu kupitia wataalam ambao wanashirikiana na timu zilizopo
katika mikoa na wilaya zilizoathirika. Mojawapo wa changamoto ni utoaji
wa idadi pungufu ya wagonjwa au kutotoa kabisa taarifa za wagonjwa wa
Kipindupindu. Hii inapelekea kusababisha mikakati iliyowekwa kutokuwa na
mafanikio hivyo ugonjwa kuendelea kuwa ni tishio katika jamii.
Ninapenda kusisitiza kuwa, taarifa za wagonjwa wa Kipindupindu zitolewe
bila kuficha, na watendaji watakaoficha taarifa za wagonjwa
watawajibishwa ipasavyo.
Changamoto nyingine iliyopo ni
ushiriki mdogo wa sekta nyingine katika kupambana na ugonjwa huu.
Ninaomba ieleweke kuwa mapambano dhidi ya Kipindupindu yatafanikiwa
ikiwa sekta nyingine kama Maji, miundombinu, biashara, elimu, mazingira
n.k zitashirikiana. Wizara yangu imeendelea kusisitiiza ushirikiano huu
katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Wilaya, ili mipango ya kupambana na
Kipindupindu ishirikishe sekta mbalimbali na pia Mashirika yasiyo ya
Kiserikali, Taasisi za Dini na Vyombo ya Habari
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269