Wachezaji
wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamezawadiwa
magari ya kifahari baada ya kushinda Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa
wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN). Rais Joseph Kabila amemtunuku kila
mchezaji gari gari la kifahari la thamani ya $60,000 (£40,000). Wachezaji
hao pia wamepewa nishani. Wachezaji wa DRC Congo walakiwa kishujaa
Chui hao wa Kinshasa walitwaa kombe kwa kulaza Mali 3-0 kwenye fainali na kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mara mbili
Mwandishi
wa BBC Mbelechi Msochi anasema mchezaji Heritier Luvumbu Nzinga
aliyeumia kwenye michuano hiyo pia ameahidiwa kwamba atasafirishwa
ng'ambo kwa matibabu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269