Breaking News

Your Ad Spot

Feb 9, 2016

MEJA JENERAL RWEGASIRA; WENYE KUMILIKI SILAHA ISIVYO HALALI WAJISALIMISHE WENYEWE POLISI TENA HARAKA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kulia) akitoka katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba, wapili kushoto ni Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza.
 Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa  Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba. Katibu Mkuu katika hotuba yake ya ufunguzi wa warsha hiyo, aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza
 Sehemu ya wajumbe wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba (wapili kushoto waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi (wapili kulia), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo (kulia) na kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa  Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Warsha hiyo ya siku mbili ilifunguliwa na Katibu Mkuu, Rwegasira katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages