Breaking News

Your Ad Spot

Feb 6, 2016

MAKAMPUNI YA HOTELI YA ZANZIBAR OCEAN VIEW KUFADHILI MICHUANO YA KIMATAIFA YA TIMU ZA JKU NA MAFUNZO KWA KUNUNUA TIKETI ZOTE ZA MICHEZO HIYO NA KUTOA BURE KWA WANANCHI KUJIONEA MICHUANO HIYO YA KOMBE LA CAF ZANZIBAR.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar BMZ  akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fedha kwa timu za JKU na Mafunzo za mchezo wao wa Kombe la CAF inayotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Meneja wa Makampuni ya Hoteli za Ocean View, Zanzibar Jacob Makundi akizungumza na Waandishi wa habari  na Viongozi na Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo (hawapo pichani) wakati wa kukabidhi fedha za ununuzi wa tiketi wa michuano hiyo inayoandaliwa na CAF Championc Leagua na Confederation Cup 2016. na kuahidi kutowa gharama zote za michezo hiyo. inayotarajiwa kufanyika feb 13 na 14 mwaka huu katika uwanja wa amaan Zanzibar.
Viongozi wa Timu za JKU na Mafunzo wakimsikiliza Meneja wa Makampuni ya Zanzibar Ocean View Zanzibar akizungumza wakati wa hafla hiyo na kutoa ahadi kwa kilia Timu ikishinda mchezo wao huo wa awali itazawadiwa shilingin Milioni Tano kwa ushindi wowote ule,wakati wa hafla ya kukabidhi fedha za tiketi za mchezo huo Kampuni yake imenunua tiketi zote zenye thamani ya shilingi miliono tano kila moja na kutowa fursa kwa Wapenzi wa mchezo wa mpira Zanzibar kuona mapambano hayo bure bila ya kiingilio.
Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo wakiwa katika hafla hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo wakiwa katika hafla hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Mshauri wa Kisheria wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Mhe Abdalla Juma akizungumza wakati wa hafla hiyo kwa niaba ya Kampuni hiyo kuhusiana na udhamini wa mchezo huo kwa timu za JKU na Mafunzo. na kutowa Salamu za Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni hayo Amani Ibrahim Makungu.
 Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhiwa  Tiketi ya Mchezo wa JKU na Gaborone United Club na Kiongozi wa Timu ya JKU Khamis Mohammed, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages