Historia ya Besigye
Kizza
Besigye Warren Kifefe alizaliwa Aprili 22, 1956, eneo la Rukungiri,
Uganda. Ni kanali wa zamani wa Jeshi la Uganda, mwenyekiti wa Forum for
Democratic Change (FDC), na amegombea katika uchaguzi wa rais nchini
Uganda mwaka 2001, 2006 na mwaka huu 2011.
Maisha ya awali na kazi
Besigye,
mtoto wa pili katika familia ya watoto sita, alisoma shule ya msingi
Kinyasano na Mbarara Junior. Wakati akiwa shule ya msingi, wazazi wake
wote walifariki. Alimaliza elimu ya sekondari katika shule ya Kitante na
baadaye sekondari ya juu katika shule ya Kigezi.
Mwaka 1975 alijiunga na Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Makerere na kufuzu shahada ya udaktari mwaka 1980.
Baada ya
kufanya kazi ya kutibu katika Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi, aliacha
na kuchukua mafunzo ya kijeshi kwa kujiunga na National Resistance Army
kati ya mwaka 1980-1986 kwenye vita vya msituni dhidi ya serikali ya
Milton Obote. Alikuwa akiwajibika kuangalia afya za wapiganaji na hasa
Mwenyekiti, Yoweri Museveni.
Yoweri
Museveni alipokuwa Rais mwaka 1986, Besigye, wakati huo akiwa na umri wa
miaka 29, aliteuliwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Mwaka 1988, aliteuliwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, na Kamisaa wa Siasa za Taifa.
Mwaka
1991, alikuwa Kamanda wa Kikosi cha kisasa wa Masaka, na mwaka 1993
akawa Mkuu wa ugavi na Uhandisi. Kabla ya kustaafu kutoka jeshi muda
mfupi kabla ya uchaguzi wa 2001, Besigye alikuwa amefikia cheo cha
Kanali na alikuwa Mshauri Mwandamizi wa Jeshi na Wizara ya Ulinzi.(VICTOR)
Mwaka
1998, Besigye alimuoa Winnie Byanyima, aliyekuwa Mbunge wa Manispaa ya
Mbarara na mwanamke wa kwanza kuwa mhandishi mwanaanga nchini Uganda.
Anselm Besigye, kijana wa kiume alizaliwa na Kizza Besigye na Winnie
Byanyima, Septemba 1999.
Uchaguzi 2001
Kabla ya
uchaguzi wa rais mwaka 2001, Besigye alijitokeza kuwa mpinzani wa sera
za NRM ya Museveni na mfumo wa serikali wa “hakuna chama”, akiamini kuwa
uongozi ulikuwa “haurekebishiki”, na kwamba “alitakiwa mtu kuchukua
hatua na kuweka mambo sawa”. Alitaka kutazamwa upya kwa mfumo wa
vuguvugu, na kubaki na utaratibu wa mpito, badala ya kuuhalalisha kama
mfumo mbadala wa siasa.
Uchaguzi
wa mwaka huo, Besigye, alionekana ndiye mpinzani pekee wa Museveni,
alikuwa mmoja wa wagombea sita, wakati wa kampeni zilizokuwa na
unyanyasaji mkubwa. Museveni alishinda uchaguzi wa urais, na matukio ya
vurugu yalitokea baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Kurudi toka uhamishoni na kukamatwa
Oktoba
26, 2005, Besigye alirejea Uganda kutoka Afrika Kusini, alikokuwa
akiishi baada ya kuondoka Uganda. Maelfu ya wafuasi wake walijipanga
mitaani kutoka Uwanja wa Ndege wa Entebbe hadi mji mkuu, Kampala.
Alikamatwa
Novemba 14, 2005, akituhumiwa kwa uhaini na ubakaji. Kesi ya uhaini
ilimhusisha na madai yake ya kuhusishwa na waasi wa vikundi vya LRA na
PRA, na mashtaka ya ubakaji ilihusishwa na madai ya tukio la Novemba
1997 kati yake na binti wa rafiki yake.
Kukamatwa
kwake kulifuatia maandamano na vurugu jijini Kampala na miji nchini
kote. Waandamanaji waliamini kuwa mashtaka yaliundwa kumzuia Besigye
kugombea rais katika uchaguzi wa 2006.
Februari uchaguzi 2006
Uchaguzi
mkuu wa 2006 ulishuhudia chama cha FDC kama chama kikuu cha upinzani na
Besigye kama mpinzani kuu dhidi ya Museveni kwenye urais. Museveni
alichaguliwa kwa kipindi kingine cha miaka mitano, kwa asilimia 59 dhidi
ya asilimia 37 za Besigye. Besigye, aliyakataa matokeo kwa madai ya
kuwepo udanganyifu.
Mahakama
Kuu ya Uganda ilitoa maamuzi kuwa uchaguzi huo ulikuwa umefunikwa na
vitisho, vurugu, kuwagawa wapigakura, na makosa mengine. Hata hivyo,
Mahakama ilimpitisha Museveni kwa kura 4-3 kuzingatia matokeo ya
uchaguzi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269