Breaking News

Your Ad Spot

Feb 9, 2016

GHOROFA LILIOANGUSHWA KWA TETEMEKO TAIWANI WAWILI WAKUTWA HAI

Mwanamke akiokolewa.
WATU wawili wameokolewa wakiwa hai kutoka kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka kufuatia tetemeko la ardhi mjini Tainan, Taiwan.Wa kwanza alikuwa mwanamke ambaye maafisa wanasema alipatikana chini ya mwili wa mumewe. Mwili wa mtoto wao wa umri wa miaka miwili ulipatikana karibu nao.
Mwanaume baada ya kuokolewa.
Muda mfupi baadaye, mwanamume pia alipatikana akiwa hai, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.Watu 37 walifariki baada ya tetemeko la ardhi la kipimo cha Richter 6.4, kukumba taifa hilo.Wengi wa waliofariki walikuwa katika jumba la Weiguan Jinlong, ambapo zaidi ya watu 100 bado wanaaminika kukwama kwenye vifusi.
Ghorofa liliporomoka
Mwanamke aliyeokolewa, Tsao Wei-ling, aliokolewa Jumatatu asubuhi, mbunge wa eneo hilo Wang Ting-yu alinukuliwa akisema na shirika la habari la Reuters.Alikuwa bado hajapoteza fahamu na alikimbizwa hospitalini.Waokoaji wanasema ni kana kwamba mwili wa mumewe ulimkinga dhidi ya nguzo iliyowaangukia.Watu 310 wameokolewa kufikia sasaJamaa watano wa familia hiyo bado hawajulikani waliko.Mwanamume huyo mwingine aliyeokolewa alikuwa akizungumza na waokoaji usiku wote kabla ya kuokolewa mchana.
Msichana wa umri wa miezi sita aliyeokolewa akiwa hai awali alifariki baadaye akitibiwa hospitalini.
Jumba la Weiguan Jinlong (Dragoni wa Dhahabu) lilikuwa na ghorofa 17. Uchunguzi unafanywa kubaini iwapo udhaifu katika ujenzi wake ulichangia kubomoka kwake.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages