Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza na Watendaji
na Viongozi wa Serikali za Mitaa wa wilaya hiyo kwenye mkutano
uliofanyika Dar es Salaam leo kuhusu jinsi ya kutatua na kukomesha kero
za ardhi
Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Makonda (hayupo pichani)
Na Dotto Mwaibale
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni ametoa siku 20 kwa Wenyeviti wote wa Serikali za
Mitaa Manispaa hiyo kuwa na ramani ya mitaa ili kuyatambua maeneo ya
wazi.
Makonda
amewataka watendaji wa Manispaa hiyo kwenda na kasi ya serikali ya
kuwatendea haki wananchi katika kumaliza migogoro ya ardhi.
Akizungumza
Dar es Salaam leo mchana na Wenyeviti zaidi ya 100 wa Serikali za Mitaa
ya9 Manispaa ya Kinondoni ,Makonda alisema baadhi ya watendaji
wanatanguliza maslahi mbele kuliko mahitaji ya Wananchi na Taifa kwa
ujumla.
Alisema
migogoro ya ardhi ni kero kila sehemu misibani, harusini na kwenye
mazishi suala kubwa ni la ardhi na kuongeza kuwa mabaraza ya ardhi ya
Kata hayana uhalali wa kuamua kesi hizo kwa kuwa baadhi yao hata uelewa
wa masuala hayo hawana na yamekuwa yakiongeza matatizo.
"Leo
tumekutana hapa kwa sababu ya migogoro ya ardhi na kuanzia sasa ndani
ya Wilaya ya Kinondoni nataka kurudisha heshima ya Wenyeviti wa Serikali
za Mitaa nawaagiza kuanzia sasa mtu yeyote kutoka Wizarani,Manispaa au
hata mwekezaji lazima apitie kwanza kwa Mwenyekiti wa Serikali ya
Mitaa,"alisema.
Alisema
watendaji wengi Manispaa ndio chanzo cha migogoro ya ardhi kwa
kutotimiza wajibu wao na wameshindwa kuonyesha dira ya kuwasaidia
wananchi.
"Kibaya
zaidi ili kujitengenezea mazingira ya ulaji wenyeviti hawashirikishwi
katika hatua za awali wanahusika zaidi pale kunapotokea
mgogoro,"alisema.
Aliongeza
kuwa "Sina hofu wala uoga wala sina sifa ya kupendwa wala kutafuta
kupendwa hivyo nitahakikisha ninatumia Mamlaka niliyopewa kufanya
migogoro hii ya ardhi Kinondoni na kuwa historia na nikitaka jambo huwa
sishindwi"alisema.
Alisema
baada ya wenyeviti hao kupewa ramani atahakikisha anakutana na Wazi ri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilium Lukuvi na maofisa wa
ardhi.
"Hapo
sasa watakaobainika kuhusika katika michezo michafu na kuchochea
migogoro basi Waziri Lukuvi aondoke nao maana wameshindwa kazi"alisema
Makonda
aliwataka wenyeviti hao kuonesha maeneo ya wazi na yale yaliyovamiwa
ili kuchukua hatua kwani wenye dhamana wapo ofisini huku wananchi wakiwa
wanateseka na migogoro hiyo.
Mkuu
wa Idara ya Mipango Miji Manispaa ya Kinondoni Juliana Letara alisema
Wenyeviti wote watapewa ramani za mitaa yao ndani ya wiki mbili kwa
kuwa zipo kwenye kompyuta ofisini hivyo atawapatia ramani hizo.
Alisema
kutokana na migogoro mingi ya ardhi anapendekeza kufanyike mapendekezo
ya mabadiliko ya sheria kwa kuwa kesi zote za mabaraza ya kata
zinaigharimu serikali zaidi ya milioni tatu kwa siku.
Alizitaja kesi hizo kuwa ni za ardhi ya hifadhi,ardhi ya kawaida na ile ya kimila
"Tulikopa
benki ya TIB mkopo kwa ajili ya kupima Viwanja likiwemo eneo la
Mabwepande lakini kila siku tunatozwa riba ya sh.milioni tatu jambo
ambalo ni gumu na ipo siku litashindikana na ndio maana tunauza Kiwanja
hadi milioni 20 na 30,"alisema.
Baadhi
ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa ambao walipata nafasi ya kuzungumza
mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo walimtaka Makonda kuondoa majipu sugu
katika Manispaa hiyo likiwemo la maofisa mipango miji.
Alisema
wako tayari kufanyazi na Makonda lakini sio wafanyakazi hao kitengo
cha ardhi kwa kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro mikubwa ya ardhi.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269