Breaking News

Your Ad Spot

Feb 7, 2016

CCM YAADHIMISHA MIAKA 39, JPM ASISITIZA WATENDAJI WA SERIKALI KUANZIA JUU HADI CHINI WATAENDELEA KUTUMBULIWA MAJIPU


Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakya Kikwete na Rais John Magufuli wakiwa wamekalia moja kati ya madawati 1,000 yaliyotolewa na CCM mkoa wa Singida ili yagawiwe kwa shule za mkoa huo ikiwa ni moja ya hatua za kutatua tatizo la madawati nchini. Walikuwa katika sherehe za miaka 39 ya CCM kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida Februari 6,2016. Watatu kushoto ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu na kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Mwenyekiti wa CCM, Rais  Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza katika sherehe za miaka 39 ya CC kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida Februari 6, 2016

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza katika sherehe za miaka 39, ya CCM kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida Februari 6, 2016

Rais Magufuli akizungumza katika sherehe za miaka 39 ya CCM kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida Februari 6, 2016.

Rais Magufuli akisalimiana na Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) mara alipowasili kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida kuhudhuria sherehe za miaka 39 ya CCM Februari 6, 2016
 Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, (kushoto), akipokewa na Nape, na katibu mkuu wa CCM Kinana

Rais Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Viti Maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Rachel Mashishanga ambaye alirejea CCM katika sherehe za Miaka 39 ya CCM kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida Februari 6, 2016


Rais Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Viti Maalum CHADEMA , Cristawaja  Mtinda ambaye alitangaza kurejea CCM katika sherehe za miaka 39 ya CCM kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida Februari 6, 2016
Wasanii wa bongo movie nao walikuwepo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages