Breaking News

Your Ad Spot

Feb 9, 2016

BENKI YA POSTA TANZANIA, TPB, YAZINDUA HUDUMA ZA KIFEDHA TAWI LAKE LA BABATI MKOANI MANYARA

Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru (katikati), akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa huduma za kifedha kwenye tawi la Benki ya Posta, Mjini Babati mkoa Manyara leo Februari 9, 2016. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, na kushoto ni Menyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi YA tpb, Profesa Lettice Rutashobya

Msajili wa hazina, Lawrence Mafuru (wapili kushoto), akimpa zawadi mmoja wa wateja wa Benki ya Posta tawi la Babati, Theofil Muhale Tsaghayo baada ya kufungua rasmi huduma za kibenki katika tawi la Babati, mkoaniManyara Februari 9, 2016. kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo Prof. Lettice Rutashobya.

Na Mwandishi wa K-VIS MEDIA, Babati


Benki ya Posta Tanzania (TPB) imezindua huduma za Kibenki kwa kufungua tawi lake jipya kwenye mji wa Babati mkoani Manyara. Akizungumza kwenye uzinduzi huo Februari 9, 2016, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Lettice Rutashobya alisema tawi lililokuwepo hapo awali halikuweza kutosheleza mahitaji ya wakazi wa Mji wa Babati na vitongoji vyake kutokana na udogo wake.

‘’Tawi hili limefunguliwa ili kutimiza dhamira ya Benki yetu ya kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wateja wake, na sasa Tawi hili litatoa huduma bora na za kisasa ikiwemo ile ya ATM kwa wafanyabiashara, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika wilaya hii ya Babati”, aliwahakikishia Profesa Rutashobya.

Profesa Rutashobya aliwashukuru wateja wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia huduma wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia huduma za Benki hiyo kwa wingi, na kulifanya tawi hilo kuwa ni mojawapo ya matawi yanayofanya vizuri kifaida.

Naye Msajili wa Hazina, Lawrence N. Mafuru, ambaye ndiye aliyezindua huduma za kibenki za tawi hilo, aliipongeza Benki ya Posta kwa kuleta maendeleo ya kuninua maisha ya Mtanzania ya hali ya chini kwa kuongeza huduma za kibenki karibu na jamii hiyo, na kwa kubuni huduma mbalimbali hususan za mikopo, zenye lengo la kumuinua kimapata mwananchi wa chini.

Msajili huyo wa Hazina, alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wakazi wa Babati kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya Posta, kwa kufungua akaunti na kwenda kuomba mikopo ambayo oinatolewa kwa riba nafuu na benki hiyo.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi amesema uamuzi wa kujenga tawi hilo ambalo linatoa huduma zote zinapatikana kwenye matawi mengine ya Benki ya Posta Tanzania nchi nzima.
“Azma ya Benki ya Posta, ni kuwafikia na kutoa huduma za kibenki kwa wananchi wote (financial Inclusion), alisema Moshingi.



Msajili wa hazina, Lawrence Mafuru na maafisa wengine wakishangilia baada ya kukata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa huduma za kibenki katika tawi jipya la Benki ya Posta, Mjini Babati mkoa wa Manyara Jumanne Februari 9, 2016. Wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Profesa Lettice Rutashobya.
Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru katika picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Pamoja na Menejimenti ya benki hiyo, baada ya ufunguzi wa huduma za kibenki katika tawi jipya la Babati, Manyara
Msajili wa hazina, Lawrence Mafuru (kushoto), akikabidhiwa kadi ya ATM ya benki ya Posta Tanzania, na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, baada ya kufungua akaunti muda mfupi baada ya kuzindua huduma za kifedha kwenye tawi la benki hiyo, Mjini Bababati mkoani Manyara Feruari 9, 2016

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages