Vikosi
vya Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM, vimesema kuwa kundi la
Al-shabab lenye uhusiano na mtandao wa kigaidi duniani wa AL-Qaeda,
limepanga kutekeleza mashambulizi nchini humo wakitumia mavazi ya
wanajeshi wa umoja huo.
Amisom
imesema katika taarifa yake kwamba mavazi hayo ya kijeshi yaliibiwa na
wapiganaji jao wa Al shabab kutoka katika kambi ya kijeshi iliochini ya
Umoja wa Afrika.
Taarifa
hiyo ya Amisom imeongeza kuwa kundi hilo limepoteza muelekeo baada ya
kuzidiwa nguvu sasa wamepanga kutekeleza mashambulizi dhidi ya raia na
vikosi hivyo.(VICTOR)
Msemaji
wa kundi hilo Aden Rage amethibitisha wapigaji wake kuwa na mavazi ya
wanajeshi wa Umoja wa Afrika na kwamba wamepanga kutekeleza mashambulizi
mfululizo ya kujitowa muhanga dhidi ya wanajeshi wa Amisom na Raia.
Kundi la
Al shabab lemye mafungamano na mtandajo wa kigaidi duniani wa Al Qaeda
limezidisha mashambulizi ya kujitowa muhanga katika siku za hivi
karibuni na limetishia kuendeleza mashambulizo hayo ya kujitowa muhanga.
Amisom
inasema ipo tayari kukabiliana na vitisho vya Al Shabab, kundi ambalo
kwa sasa limepoteza nguvu kubwa baada ya kusambaratishwa katika miji
kadhaa iliokuwa ikikalia.CHANZO:RFI
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269