Breaking News

Your Ad Spot

Nov 22, 2015

MTANZIKO WA KISIASA ZANZIBAR NA SWALI LA LA ZANZIBAR KUNA RAIS AU LA...?

















Ndugu zangu,
Utata wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar na matokeo yake umeleta mtanziko wa kisiasa.
Nina bahati ya kufuatilia kwa karibu siasa za Zanzibar tangu nikiwa Sekondari. Siasa za Visiwani haziwezi kabisa kufananishwa na za Bara.
Tuliowaona jana wakizomea Bungeni yumkini wengi wao walikuwa kwenye mkumbo wa kuzomea wasichokijua.

Kuna waliowaaminisha wenzao kuwa Zanzibar hakuna Rais! Ni kweli kuwa Zanzibar kuna mtanziko wa kisiasa, lakini kwamba Zanzibar hakuna Rais na Serikali hilo si la kweli.
Kwa ufupi tu, na kwa mujibu wa Katiba yao Zanzibar, kama Rais mpya hajapatikana, basi aliyepo ndiye atabaki kuwa rais mpaka mpya apatikane na aapishwe. Hatupaswi kujitia ujinga na upofu tushindwe kuliona hilo la kisheria na kikatiba.
Wenye kusema Zanzibar hakuna Rais wala Serikali wanajua fika kuwa hilo halipo. Kila kukicha, na hata kesho kukicha, Wazanzibar wataendelea kupata huduma za Kiserikali. Hivyo, inamaanisha uwepo wa Serikali na Uongozi wa Kiserikali.
Hata hivyo, ukweli huo haufuti hali ya mtanziko wa kisiasa uliopo visiwani, na wenye kuhitaji suluhu kwa njia ya mazungumzo ya pande husika hadi wafikie muafaka. Hilo ni la Wazanzibar wenyewe, ingawa, siku zote, na kwa historia, jambo la Zanzibar ni letu Bara na kinyume chake.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages