Breaking News

Your Ad Spot

Nov 18, 2015

MISS TANZANIA 2014 KUKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA TAREHE 19 NOV 2015

1430651368__mg_0081.jpg
Mrembo wa Taifa Miss Tanzania Lilian Deus Kamazima atakabidhiwa Bendera ya Taifa na Mkuu wa Mkoa wa DSM ikiwa ni ishara ya kumtakia kila la heri katika mashindano ya urembo ya Dunia yatakayofanyika Sanya China tarehe 19 Desemba 2015.
Mrembo huyo ataondoka nchini Ijumaa ya tarehe 20 Novemba 2015 na ataungana na waremboe wengine kutoka nchi zaidi ya 120 duniani  na watapiga kambi ya mwezi mmoja katika Hotel ya Beuaty Crown Sanya China.
Miss Tanzania Lilian amekuwa katika maandalizi ya kutosha tangu achukue Taji hilo mwezi Oktoba 2014
Pamoja na mambo mengine ameshiriki  Onyesho la Mavazi la nchi za Afrika ya Mashariki lililoandaliwa na Kampuni ya Arapapa Fashion ya mjini Kampala Uganda mwezi Novemba 2014.
Ameshiriki katika shughuli mbalimbali za Jamii katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na D’salaam.
Kama Balozi wa Hospital ya CCBRT Miss Tanzania Lilian anaondoka na ujumbe wa kupiga vita na kupambana na matatizo ya wasichana na akina mama ya Fistula.
Mrembo huyo anatarajia kurejea nchini tarehe 20 Desemba 2015.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages