Breaking News

Your Ad Spot

Nov 18, 2015

MAMBO MATATUYA KUFAHAMU KUTOKA SIMBA, KUHUSU MAVUGO, HASSAN KESSY NA KIONGERA

Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba imekuwa ikihusishwa kwa mambo kadhaa sasa kuhusiana na dirisha dogo la usajili, wengi wamekuwa wakiitaja Simba kuwa kwa sasa haina mshambuliaji mkali zaidi ya Hamisi Kiiza hivyo huenda ikamsajili mrundi Laudit Mavugo katika dirisha hili kutokana na tetesi kuwa mkataba wake una malizika na klabu ya Vital’O.
Stori zimekuwa nyingi ikiwemo taarifa ya kumrejesha mshambuliaji wake Paul Kiongera raia wa Kenya waliyekuwa wamemtoa kwa mkopo Kenya ila sasa anarejea, millardayo.com ilimtafuta Mkuu wa Idara ya Habari wa Simba Haji Manara azungumzie mambo matatu, kuhusu kumsajili Laudit Mavugo, mkataba wa Hassan Kessy na nani atarithi mikoba ya Selemani Matola katika nafasi ya ukocha msaidizi atatoka nje ya nchi au?
“Kessy bado ana mkataba wa miezi saba na Simba hivyo hakuna klabu inayoruhusiwa kuongea nae sababu bado mchezaji wa Simba na akirejea kutoka Algeria tutamuongezea mkataba” >>> Manara
DSC_0044
“Kiongera ndio anarudi kuhusu mshambuliaji mpya ndio tuna mpango huo ila subirini tutawaambia kama ni Mavugo mtajua tu ila ndani ya siku mbili hizi Kiongera ataanza mazoezi na wenzake” >>> Manara
“Kweli tumtafuta kocha msaidizi ila ni ndani ya nchi kuhusu nani kapendekeza ni kamati ya utendaji mwalimu yeye anatoa maoni ambayo yanabakia ndani ya klabu ila Simba ndio ina maamuzi ya kumchagua kocha msaidizi hivyo wakati wowote kutokea sasa

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages