Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (wa kwanza
kushoto) akiangalia mitambo ya kurushia matangazo ya Shirika la
Utangazaji Tanzania(TBC) wakati alipofanya ziara ya kikazi katika minara
ya shirika hilo leo hii Kisarawe.Profesa Elisante amefanya ziara katika
Taasisi tatu zilizo chini ya Wizara hiyo ambazo ni Baraza la Sanaa
Tanzabia (BASATA),Tanzania Standard Newspapers (TSN) na Shirika la
Utangazaji Tanzania(TBC) lengo likiwa ni kufahamiana na
wafanyakazi,kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii na kujua changamoto
zinazowakabili ikiwa ni kutimiza kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya awamu ya
Tano.Anaefuatia ni mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw.Clement Mshana.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiangalia
tofauti ya santuri ya zamani na flashi ya kisasa zinavyozidiana ukubwa
kwa umbo alipotembelea maktaba mojawapo katika ofisi za shirika la
utangazaji Tanzania (TBC) alipofanya ziara kuongea na menejimenti ya
shirika ilo leo jijini Dar es Salaam.Santuri zilitumika kipinda shirika
hilo likiitwa Radio Tanzania Dar es Salaam.(RTD).
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(waliosimama
watatu kulia) akiwa katika mojawapo ya studio za kurushia matangazo ya
shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wwakati alipotembelea shirika ilo
leo kuongea na menejimenti yake pamoja na kuona utendaji wake.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(aliyekaa
mwenye miwani) akipata maelekezo jinsi gazeti linavyotengenezwa kutoka
kwa mtumishi wa Standard News Papers(TSN) leo jijini Dar es Salaam
alipofanya ziara ya kikazi na kuangalia utendaji wa kazi.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (wa pili
kulia) akiangalia moja ya kazi za vijana wanojifunza kutengeneza batiki
na kuweka chapa alipotembelea ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA)
leo hii jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269