Breaking News

Your Ad Spot

Nov 13, 2015

JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO THAILAND WAMCHAGUA BW. MAUMBA MGAYA KUWA MWENYEKITI WA TIT

Meza Kuu , Kutoka Kushoto ni Ndugu Maumba Mgaya, Mwenyekiti wa Jumuiya, Bi Magreth Mjindo na Ndugu Andrew Katibu
Meza Kuu , Kutoka Kushoto ni Ndugu Maumba Mgaya, Mwenyekiti wa Jumuiya, Bi Magreth Mjindo na Ndugu Andrew Katibu.
Mnamo tarehe 7/11/2015, Jumuiya ya watanzania waishio nchini Thailand ilikutana na kujadiliana mambo mbalimbali ya jinsi gani wanaweza kusaidiana katika mambo mbalimbali, TIT ilianzishwa mnamo mwezi wa nne mwaka, 2015 na inahusisha watanzania mbalimbali, wanafunzi, wafanyabishara na wafanyakazi waishio na kufanya nchini Thailand. Mkutano mkuu wa Jumuiya ulifanyika katika Hoteli ya Amari Boulevard Mjini Bangkok na kuhudhuriwa na wanajumiya mbalimbali.
Pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali kulifanyika uchaguzi wa viongozi ambapo wafuatao walichaguliwa kuwa viongozi wa jumuiya kwa kipindi cha mwaka mmoja:

Mwenyekiti: Bwana Maumba Mgaya
M/Kiti: Bw. Alois Ngonyani
Katibu: Bw.Andrew Wajama
Katibu Msaidizi: Bw. Emmanuel Mushi
Mhazini: Bw. Adolf Kigombola
Mhazini Msaidizi: Bi.Tumaini Kalindile
Afisa Mawasiliano: Bw. Emmanuel Nyamageni
Afisa Mawasiliano Msaidizi: Bw. Jordan Hossea.

Pamoja na uchaguzi kulifanyika sherehe fupi ya kumpongeza Bi Magreth Dionis Mjindo ambaye amemaliza Shahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii na anarejea nyumbani kulitumikia Taifa.
Jumuiya inapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wao Ndugu Florean Rwehumbiza, Dada Lucy Kileo pamoja na Ndugu Kivea Mbwana (Homeboy) kwa kusimamia uchaguzi na kufanikisha kufanyika kwa mkutano huu muhimu. Shukrani za pekee ziende kwa Kampuni ya Broadhurst Pacific, kwa kusimamia, kudhamini na kufanikisha tukio hili muhimu.
Mhazini wa Jumuiya Ndugu Adolph Kigombola akisoma taarifa ya fedha
Mhazini wa Jumuiya Ndugu Adolph Kigombola akisoma taarifa ya fedha.
Tunapenda kuwapongeza na kuwashukuru viongozi waasisi wa jumuiya waliomaliza muda wao ambao ni ndugu Saidi Husein Kitenge Mwenyekiti wa kwanza wa jumuiya na makamu wake Ndugu Masui Vicent Munda na ndugu Antidius Muchunguzi bila kuwasahau maafisa mawasiliano wetu akiwemo ndugu Felix Mwema na Bi Diana Richard.Mungu awabariki kwa kuitumikia vema TIT.
Aidha Jumuiya inawakaribisha watanzania mbalimbali walioko nchini Thailand au wanaotarajia kuja nchini Thailand kushirikiana na jumuiya yetu.
Umoja ni nguvu
Imetolewa na Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Thailand (TIT)
+66947230002/+66972494819
Mkutano Mkuu Ukiendelea
Mkutano Mkuu ukiendelea.
Baadhi ya Watanzania Waishio nchini Thailand
Baadhi ya Watanzania Waishio nchini Thailand.
Mkutanoni
Mkutanoni.
Timu ya Wadhamini wakisimamia Uchaguzi
Timu ya Wadhamini wakisimamia Uchaguzi.
Bw. Florean Akikabidhiwa keki ya kuzaliwa na Bi Lucy
Bw. Florean Akikabidhiwa keki ya kuzaliwa na Bi Lucy.
Ndugu Florean akimkabidhi Bi Magreth Zawadi kwa niaba ya Jumuiya
Ndugu Florean akimkabidhi Bi Magreth Zawadi kwa niaba ya Jumuiya.
Wanajumuiya Wakipata Chakula cha Pamoja
Wanajumuiya Wakipata Chakula cha Pamoja.
Watanzania Waishio Thailand wakipata chakula cha pamoja
Watanzania Waishio Thailand wakipata chakula cha pamoja.
Watanzania Waishio Thailand Wakiwa Katika Picha ya Pamoja
Watanzania Waishio Thailand Wakiwa Katika Picha ya Pamoja.
EPVI3455

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages