Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)
limetangaza kuwa idadi ya wakimbizi raia wa Mali wanaokimbilia nchini
Niger imeongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Msemaji wa UNHCR, Leo Dobbs amesema, katika kipindi cha kati ya mwezi
Oktoba hadi mwanzoni mwa mwezi huu wa Novemba idadi ya wakimbizi kutoka
Mali waliokimbilia nchini Niger imeongezeka na kufikia 4,000, kiwango
ambacho ni cha juu zaidi tangu yalipozuka mapigano nchini Mali mwaka
2012 hadi sasa.
Dobbs ameongeza kuwa kwa sasa idadi ya wakimbizi hao imefikia watu
54,000 na kuna wakimbizi wengine 3,000 wanaotarajiwa kuongezeka.
Msemaji wa UNHCR amefafanua kuwa licha ya serikali ya Mali na
wapinzani wanaobeba silaha kusaini makubaliano ya amani mwezi Juni mwaka
huu baada ya duru kadhaa za mazungumzo chini ya upatanishi wa Algeria
lakini kumekuwepo na matukio kadhaa ya ukiukaji makubaliano hayo na
mapigano ambayo yamekuwa yakishuhudiwa katika maeneo ya kaskazini mwa
Mali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269