Breaking News

Your Ad Spot

Nov 26, 2015

HAKIELIMU YAZINDUA JOPO LA WASHAURI MABINGWA

Timu
ya Menejimenti ya HakiElimu ikiwa katika picha na Mwenyekiti wa Bodi ya
HakiElimu na Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa jopo la washauri
bingwa
Wafanyakazi wa Shirika la HakiElimu waliohudhuria uzinduzi katika picha ya pamoja na jopo la washauri bingwa
Waliosimama ni Prof. J. Galabawa (kushoto) Prof. Kitila Mkumbo (katikati) na Prof. Elias Jengo (kulia) Waliokaa ni John Kalage (Mkurugenzi wa HakiElimu) Prof. G.Mmari (katikati) na Prof. Prof. Martha Qorro (Kulia).
Mgeni
rasmi Prof. Geofrey Mmari,akizungumza jambo katika hafla fupi ya
uzinduzi wa jopo la washauri mabingwa akitoa neno la ufunguzi.
Prof. Kitila Mkumbo mmoja wa wajumbe wa ThinkTank akitoa neno kwa niaba ya jopo la washauri bingwa wa HakiElimu.
Mwakilishi
wa Kamishna wa Elimu Bi, Joyce Sekimanga kutoka Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi akiwasilisha ujumbe kutoka serikali katika uzinduzi wa
jopo la washauri wa HakiElimu
Prof. Martha Qorro mmoja wa wajumbe wa jopo la washauri
mabingwa akipokea mpango mkakati wa HakiElimu kutoka kwa mgeni Rasmi
Prof Geofrey Mmari
Prof. J. Galabawa mmoja wa wajumbe wa jopo la washauri mabingwa akipokea mpango mkakati wa HakiElimu
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu John Kalage akielezea lengo la kuanzishwa kwa Think Tank
Washiriki katika uzinduzi wa jopo la washauri mabingwa wa HakiElimu
…………………………………………………………………………………….
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 
SHIRIKA la HakiElimu
limezindua Jopo la Washauri Mabingwa
linaloundwa na maprofesa 10 waliobobea katika fani ya elimu ili  kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa
watoto kupata elimu bora.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu , John Kalage amesema kazi ya jopo
hilo itakuwa kutoa ushauri wa kitaalam juu ya masuala ya elimu kadri
litakavyoombwa na  HakiElimu.
 
Amesema jopo hilo litatatoa ushaufri juu ya mikakati
,taratibu na mbinu za kuhakikisha ushiriki madhubuti katika kukuza na kutetea
ubora wa elimu nchini.
 
Kalage aliwataja maprofesa wanaounda jopo hilo kuwa ni
Abel Ishumi,Herme Mosha,Justinian Galabawa,Kitila Mkumbo,Suleiman
Sumra,Martha  Qorro, Mwajabu
Possi,Akundaeli Mbise, Masalukulangwa pamoja na Elias Jengo.
 
Amesema kuanzishwa kwa jopo hilo litasaidia shirika
kupata mawazo mapana zaidi ya kitafiti na uchambuzi wa changamoto za sekta ya
elimu.
 
Kalage amesema kuwa jopo hilo litakwenda sambamba na
jitihada za serikali kuwa na mikakati mingi ya kuboresha elimu na azma ya
serikali kutekeleza maazimio mbalimbali ya kimataifa kama  Malengo Maendeleo Endelevu (SDGs)na Incheon ya
uboreshaji wa elimu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages