Breaking News

Your Ad Spot

Nov 19, 2015

DR. TULIA ACHAGULIWA KUWA NAIBU SPIKA 71.2%

TULIA
Aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson Mwansasu hivi punde amechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata jumla ya kura 250 sawa na 71.2% huku mpinzani wake Magdalena Sakaya (CUF) akipata kura 101 sawa na 28.8%.
Dk. Tulia hivi karibuni aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kuwa mbunge baada ya kutenguliwa uteuzi wake kama Naibu Mwanasheria Mkuu.
Kabla ya uteuzi huo, Dk. Tulia alikuwa akiwania nafasi ya Uspika wa bunge baada ya kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini yeye na mgombea mwenzake Abdullah Ali Mwinyi walijitoa na kumuachia Job Ndugai awanie nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages