Breaking News

Your Ad Spot

Oct 7, 2015

DK. MAGUFULI AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE

????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiongozana na Mama Napono Sokoine mke wa  Waziri Mkuu wa Tanzania Marehemu Edward Moringe Sokoine mara baada ya kuwasili nyumbani hapo Monduli juu kwa ajili ya kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu na kukagua nyumba ya familia inayojengwa na serikali ili kuboresha makazi ya familia ya marehemu Edward Moringe Sokoine.
????????????????????????????????????
Kaburi la Marehemu Edward Moringe Sokoine.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiongozana na Mama Napono Sokoine na mtoto wa marehemu Sokoine Namelok Sokoine kwenda kuweka shada la maua katika kaburi hilo.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akishiriki sala ya kumuombea marehemu wakati walipofika nyumbani kwa Marehemu Edward Sokoine na kuweka shada la maua katika kaburi lake.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Edward Moringe sokoine huko Manduli juu wakati alipoitembelea familia hiyo.
????????????????????????????????????
Mke wa Marehemu Edward Moringe Sokoine mama Napono Sokoine akisaidiwa kuweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe Edward marehemu Moringe Sokoine.
????????????????????????????????????
Namelok Sokoine ambaye pia ni mgombea ubunge wa jimbo la Monduli naye akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu baba yake Edward Moringe Sokoine.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli , Mama Napono Sokoine kushoto na Namelok Sokoine wakishiriki ibada ya kumuombea marehemu huko Monduli juu wakati Dk. John Pombe Magufuli alipokwenda na kuweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Edward Sokoine.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiongozana na mtoto wa marehemuEdward Moringe Sokoine Namelok mara baada ya kuweka shada la maua kaburini.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanajeshi wanaofanya kazi ya ujenzi wa nyumba ya familia ya Sokoine inayojengwa na serikali wakati alipotembelea makazi ya familia hiyo.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na familia ya marehemu Sokoine na baadhi ya wafanyakazi wa Suma JKT mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba hiyo. 
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiagana na Mama Napono Sokoine mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Sokoine na kukagua ujenzi wa nyumba ya familia hiyo inayojengwa na serikali.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages