Breaking News

Your Ad Spot

Aug 7, 2015

WASANII WA FANI MBALIMBALI TANZANIA WAMUAGA RAIS KIKWETE KWA DINNER MAALUM, WAMTEUA KUWA SHUJAA WAO

Na Bashir Nkoromo, theNkoromo Blog
Wasanii wa fani mbalimbali jana kuanzia jioni walijumuika na Rais Jakaya Kikwete katika chakula cha jioni, kwa ajili ya kuagana naye, kufuatia kukaribia kumaliza mda wake wa urais.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, pamoja na Rais Kikwete, ilihudhuriwa pia na Mgombea mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Jakaya Kikwete alisisitiza kuwa wasanii ni watu muhimu ambao kazi zao zinapaswa kulindwa ili ziwanufaishe kama ilivyo kwa wasanii wengine duniani kama walioko nchi kama za Marekani.

Rais Kikwete aliahidi kuendelea kusaidia juhudi za kuwafanya wasanii waishi maisha yaliyo bora kwa kupata kipato kinacholingana na kazi zao hata akishastaafu nafasi yake ya urais.

Ili kutekeleza azma yake hiyo, Rais Kikwete aliahidi kuwa mlezi wa wasanii ili kuwewezesha masuala yao mengi yapige hatua zaidi.

Mapema wasanii walimtawaza Rais Kikwete kuwa Shujaa wao, na kumtunuku picha maalum iliyonakshiwa karibu majina ya wasanii wote nchini, Picha hiyo alikabidhiwa na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Nikki wa Pili ambaye kabla ya tukio hilo, alieleza jinsi tasnia ya sanaa, inavyochangia pato la taifa na changamoto zinazowakabili wasanii.

Katika hafla hiyo, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye walichangamsha ukumbi, baada ya kupanda jukwaani na kuzicharaza ala za muziki kwa umahiri mkubwa.

Dk. Magufuli aliamsha hoihoi ukumbini kwa kuzicharaza tumba, huku Napa akicharaza gita zito la Bess, na wote kuunogesha moja ya nyimbo za zamani, wa DDC Mlimani Park  ulioimbwa na msanii, Recho.

Baadhi ya wasanii wengine waliotumbuiza ni Farid Kubanda (Fid Q), Shakila, Rud, Jose Mara.

 Rais Jakaya Kikwete akiingia katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, kuhudhuria chakula cha jioni, kilichoadaliwa kwa ajili ya Rais Kuagana na wasanii wa fani mbalimbali hapa nchini, jana usiku. Pamoja naye ni Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.
---------------------------------
HABARI KATIKA PICHA
 Rais Jakaya Kikwete na viongozi aliofuatana nao wakiwa wamewasili ukumbini na zifuatazo ni picha mbalimbali za wasanii waliohudhuria ukumbini
 Kassim Mponda akiwa na wenzake maarufu
 Mzee Kingi Kikii akiwa na wenzake maarufu
 Rais Kikwete  akimsalimia Mzee Yusuf kwa furaha
 Akimsalimia pia mke wa Mzee Yussuf
 Mzee Yussuf akapata fursa ya kuteta jambo Rais Kikwete
 Wasanii wakijipiga picha kwa simu na Rais Kikwete wakati akiwasalimia
 Rais Kikwete akiwasalimia kwenye meza ya Kina Baba Zoro
 Rais Kikwete alifurahi kiasi cha kukumbatiana na baadhi ya wasanii, kama alivyofanya hapa 
 Rais Kikwete akiendelea kusalimia wasanii meza moja baada ya nyingine
Akafika hadi meza aliykuwepo Madam Rita wa Bongo Star Search
 Nao wakapata fursa ya kujipiga picha na Rais kwa kutumia simu yao
 Rais akafika hadi kwa Juma Kaseja
 Salam zikaendelea
 Rais Kikwete akajitahidi kusalimia kila mmoja na zifuatazo ni picha mbalimbali za wasanii wakiwa kwenye meza zao
 Wasanii wakiwa wameketi kwa utulivu mezani


Mwanamuziki Waziri Ally (kulia) akifurahia jambo
Wanamuziki wakongwe wa muziki wa Taarab, Patricia Hilary  Bi Shakila wakifuatilia hali ya mambo ukumbini
 Fid Q akiwa ndani ya nyumba
 Wengine wakiwa katika nyuso za kutafakari hali ya mambo
 Wengine wakiendelea na vinywaji
 Wasanii wakijichanganya bila kujali fani zao
 Ally Chocky (kushoto) ndani ya nyumba
 Diamond Platinum akisalimia wenzake baada ya kuingia ukumbini
 Jay B (kushoto) pia ndani ya nyumba
 Baadhi ya wakurugenzi wa vyombo vya habari wakiwa ndani ya nyumba. hapo kuna Benny Kissaka (kushoto) na kulia ni Danny Chongolo
 Rey naye ukumbini
 Mzee Yussuf na mkewe wakiwa ndani ya nyumba
 Kina Juma Kaseja ndani ya nyumba


 Msanii Rubby akiimba wimbo maalum wa kuisifu Tanzanaia
 Fid Q akiimba kutumbuiza ukumbini
 Jose Mara akiimba wimbo wa Mbaraka Mwishehe wa kuisifia Morogoro
 Diamond akitoa tamko kuhusu tasnia ya Sanaa, alisema, kabla ya umaarufu aliwahi kudandia kampeni za CCM kutoka Mwanza hadi Dar, hadi akatambuliwa


 Rais Kikwete uso kwa uso na Msanii na Msanii King Majuto
 Bi Shakira akiimba wimbo Macho yanacheka Moyo unalia


 Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Magufuli akizicharaza tumba, huku Nape akicharaza Bess
 Recho akiimba wimbo wa Sikinde
 Msanii Wema Sepetu, akimtunza Dk. Magufuli Dola za marekani baada ya kuvutiwa anavyocharaza tumba
 Jay B na Mwana FA wakiwa wamekaribishwa kuketi meza kuu
 Bushoke akiimba wimbo wake wa maarufu wa kunyanywaswa na mke
 Shughuli hiyo ikamfikisha Hussein Bashe katikati ya Nape na Kinana
 Kinana akimshauri jambo Bashe
 Rais Kikwete akipata picha na Fid Q
 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akisakata mzuziki na Madam Rita
 Rais Kikwete akisakata muziki katikati ya wasanii
 Nikki wa pili akitoa maelezo kabla ya kumkabidhi Rais Kikwete picha maalum
Rais Jakaya Kikwete akikabidhiwa picha maalum yenye majina ya wasanii karibu wote, kutoka kwa Nikki wa Pili. Kulia ni Fid Q. Picha zote na Bashir Nkoromo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages