Breaking News

Your Ad Spot

Aug 12, 2015

TUJIFUNZE KUTOKA KENYA – USALAMA MITANDAO

Nimekamilisha vikao vya usalama mitandao vilivyofanyikia jijini Nairobi kufuatia mualiko maalum nilioupata. Katika vikao hivyo niliwasilisha mada mbili (ya kwanza ikiwa ni namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao na mada ya pili ikiwa ni namna ya uchunguzi wa makosa ya digitali kitaalam) katika mada hizo mbili ambazo zilipokelewa vizuri na kupelekea mijadala ya kipekee kuna mengi  nikajifunza kutoka kwa washiriki. Aidha, nilishiriki mijadala duara iliyojikita katika changamototo mbali mbali za uhalifu mitandao na kuiangazia sharia mtandao ya nchi ya Kenya.
Kenya ni miongoni mwa nchi tatu barani afrika ambazo zimeorodheshwa kua na uhalifu mkubwa sana wa kimtandao nyingine ni Nigeria pamoja na Afrika ya kusini. Tukijadili takwimu za kutisha duniani kote, tulishuka na kuangazia bara la Afrika na baadae Afrika mashariki na hatimae kujikita na twakwimu za Nchi ya Kenya.
Kwa upande wa Kenya kwa mujibu wa takwimu zilizo wasilishwa katika mkutano, hadi kufikia Mwezi wa saba mwaka huu (2015) kuna simu 34.8 Milioni  huku watumiaji wakiwa ni 26.0 Milioni. Aidha, matumizi ya intaneti ni 29.1 milioni ambayo ni sawa na 65% “penetration”. Takwimu hizo zinasindikizwa na upotevu wa dola za kimarekani 20 milioni ($20 Mil) kila mwaka kutokana na uhalifu mtandao.
Palizungumzwa matukio ya kudukuliwa kwa tovuti Nchini humo ambapo, tovuti za serikali 103 ziliathiriwa mwaka 2013, na 3 kwa mwaka wa 2014 huku twitter ya serikali mwaka jana (2014) ikiwa ni miongoni mwa zilizo dukuliwa na kutumiwa vibaya. Nilihoji tofauti kubwa ya udukuzi wa tovuti na kujulishwa baada ya tukio la aina yake la mwaka 2013 serikali iliamua kuzifunga tuvuti zake nyingi hasa zile zilizo onekana hazina umuhimu sana kua hewani kitu ambacho kilichangia kupunguza namba kubwa ya udukuzi kwa mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages