Breaking News

Your Ad Spot

Aug 28, 2015

TAMASHA LA MANUNUZI KUFANYIKA JUMAMOSI





Na Mwandishi Wetu

TAMASHA la manunuzi maarufu kama Pop Up Bongo, ambalo limeandaliwa na kampuni ya Studiored PR linatarajiwa kufanyika Jumamosi (Agosti 29) katika baa ya Triniti iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana hadi 2 usiku.

Tamasha hilo linalodhaminiwa na kampuni ya Smirnoff, ni la kwanza na la aina yake kufanyika jijini ambapo linafungua duka la muda mfupi la manunuzi ya rejareja ambapo wanunuaji watapata fursa kwa siku moja tu katika eneo maalum.

Maduka ya Pop Up duniani kote yanafanya mauzo ya rejareja kwa kuwapa wateja uzoefu wa manunuzi mbadala na wa ubunifu ambao ni tofauti kwa maduka ya rejareja yaliyozoeleka.

Aidha, bidhaa zitakazouzwa zitaleta shamrashamra nyingi, ufahamu na kuwapa wateja msisimko wenye furaha na wa kipekee kufanya manunuzi. Tamasha hilo  linafanyika kila baada ya miezi mitatu hadi minne katika maeneo mbalimbali huku bidhaa mpya zikiuzwa katika kila tukio.

Hii ni fursa kwa ajili ya wajasiriamali wa ndani kuweza kutangaza bidhaa zao na  kuweza kujulikana huku sekta ya fasheni na mtindo wa maisha ikizidi kukua.

Kampuni zenye bidhaa zitakazokuwa kwenye tukio hilo ni pamoja na; Secret Habits, Enjipai, PSJ Couture, Dress Kitenge, Africology, Kaya African Collection, OGS Studio, Nuya’s Essence, Henna Hub, FT Boutique na Branoz Collections, Happy Socks, Kipilipili pamoja na DJ Vasley, ambaye atampa kila mtu burdani huku wakifanya manunuzi kwa siku nzima.

Onesho la Pop Up Bongo lilizinduliwa Juni 28, 2014 katika eneo la Terrace Slipway, ambako tukio lililopewa jina la "Lipstick & Lace" likishirikisha wauzaji wawili wa rejareja- Secret Habits na Atsoko.

Ni tukio ambalo lilipata mahudhurio mazuri, ambapo wateja 70 hadi 80 waliitumia alasiri ile kwa kufanya manunuzi na kuburudishwa na muziki pamoja na tafrija na vinywaji. Tukio la Pop Up Bongo kwa sasa lina wahudhuriaji zaidi ya 400 na kampuni za bidhaa 15.

Majira haya ya joto, tunakuletea tukio la 5 la Manunuzi la Pop Up Tanzania na bidhaa zako uzipendazo. Kipya katika kipindi hiki ni ni "Huduma Maridhawa", ambapo wageni wanaweza kupata vinywaji ambavyo vitabuniwa na kutolewa bure baada ya kununua chupa ya Smirnoff.

Pia kipya ni nembo ya biashara ya Pop Up Polaroid ambayo itawapa wageni fursa kupata machapisho ya Polaroid ambayo wanaweza kutumiana katika akaunti zao za mitandao ya kijamii na kuweka kama kumbukumbu ya tukio hilo

"Hii ni jukwaa la kuuza bidhaa yako kuvuma kipeke nchini Tanzania. Tunataka kuwasaidia wajasiriamali wa ndani katika sekta kukua, kupata wateja wapya na pia pesa "anasema Natasha Stambuli, muasisi mwenza wa Pop Up Bongo.

Duka la siku moja la Pop Up  linaunda jukwaa kwa ajili ya fasheni mbalimbali na mitindo ya maisha ya kampuni za bidhaa mbalimbali kuweza kuonesha bidhaa zao na kushirikiana na wateja huku wakifurahia alasiri ya kusisimua wakifanya manunuzi, kucheza muziki na kupata vinywaji.

Natasha Stambuli, muasisimwenza wa Kampuni ya Pop Up Bongo na mmiliki wa moja ya kampuni za kijasirianali zinazoshiriki, Tabia Siri, ana shauku ya kupenda kazi za kijamii. Yeye ni mmoja wa wanachama wa Chama cha Umoja wa Mataifa cha Tanzania, akifanyakazi pamoja nao kukusanya fedha za kununua vitanda kwa ajili ya wodi za wazazi nchini Tanzania. Kwa sababu hiI, Sh 1,000 ya kila mauzo itachangia kwa ajili hiyo.

Tukio la Pop Up Bongo linaandaliwa na Studiored PR na limeasisiwa na waanzilishiwenza wengine, Tanya Mulamula na Natasha Stambuli.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages