Breaking News

Your Ad Spot

Aug 23, 2015

SIMBA SC ‘IMEJIKOSESHA’ YENYEWE NDAYISENGA, HAKUWA WA DAU KUBWA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
DAU la mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Kevin Ndayisenga aliyetaka kusajiliwa Simba SC lilikuwa chini ya dola za Kimarekani 50,000 na si 70, 000 kama ilivyoelezwa awali.
Kwa mujibu wa habari za kiuchunguzi, ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE imezipata, Ndayisenga ni mchezaji huru ambaye Simba SC ilipaswa kumalizana na wakala wake tu, Dennis Kadito.
Hata hivyo, baada ya kikao baina ya Simba SC na Kadito, pande hizo mbili hazikukubaliana na mchezaji huyo akaondoka.
Habari zinasema, Simba SC ilitaka kutumia dola 35,000 (Sh. Milioi70) kwa usajili mzima wa mchezaji huyo maana yake ni kiasi kidogo wangeongeza wangeweza kumpata
Kevin Ndayisenga (kushoto) alicheza vizuri na kufunga Simba SC ikiilaza 2-1 URA Jumamosi ya wiki iliyopita
Ndayisenga.
Lakini mchezaji huyo ameondoka juzi na Simba SC imemleta mpachika mwingine kutoka Senegal, Papa Niang.
Mchezaji huyo kutoka klabu ya Alianza F.C. ya El Salvador ambaye ni mdogo wa mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Senegal, Mamadou Niang na awali alichezea timu za CF Mounana ya Gabon, Al Shabab SC ya Kuwait, FC Vostok ya Kazakhstan, FF Jaro, AC Oulu na FC OPA za Finland.
Ikumbukwe, Ndayisenga alikuwa mpango mbadala baada ya Simba SC kumkosa mshambuliaji mwingine hatari wa Vital’O, Laudit Mavugo kufuatia klabu mbili za nchini humo kupandisha thamani ya mchezaji huyo na kuwa Sh. Milioni 200, badala 110 zilizokubaliwa awali.
Aidha, kuibuka pia kwa mzozo mpya kati ya klabu ya Vital’O FC na Solidarity FC, inayodai kumlea Mavugo na kudai ina hakimiliki ya mchezaji huyo nako kuliishitua Simba.
Vital’O ikaikoroga zaidi Simba SC baada ya kudai kiwepo kipengele cha wao kupata asilimia 50 kama mchezaji huyo atauzwa na Wekundu hao wa Msimbazi kwenda klabu nyingine

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages