Breaking News

Your Ad Spot

Aug 5, 2015

RAIS KIKWETE ATIA SAINI KURIDHIA MISWADA YA SHERIA MITANO HADHARANI IKULU , DAR ES SALAAM

1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava.
2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava.
3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonga muhuri wake hati ya Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava.
4
Rais Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene baada ya kuweka saini kuridhia  Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kuridhia Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya na Katibu Mkuu wizara hiyo  Dkt. Servacius Likwelile.
7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Katibu Mkuu Waziri wa Fedha Dkt. Servacius Likwelile baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
  sa6
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
sa8
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Dkt. Shukuru Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo Profesa Sifuni Mchome.
sa9
11
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  Profesa Sifuni Mchome baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
sa10
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam kulia ni  Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo Profesa Sifuni Mchome.
12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Mheshimiwa George Simbachawene, Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Saada Mkuya, Waziri wa Fedha na Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa,  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi baada ya hafla ya kuweka saini na kuridhia miswada ya  Sheria ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Uwazi na Uwajibikaji, Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Masoko ya Bidhaa na Muswada wa Tume ya Walimu.
PICHA NA IKULU
…………………………………………………..
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
New Picture
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Agosti 4, 2015, ametia saini Miswada ya Sheria mitano hadharani ikiwa ni hatua yake ya mwisho kabisa kuridhia Miswada ya Sheria akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika sherehe iliyofanyika katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam,Rais Kikwete ameridhia Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Uwazi na Uwajibikaji, Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Masoko ya Bidhaa na Muswada wa Tume ya Walimu.
Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na mamia ya wageni waalikwa, mawaziri wanaohusika na sekta hizo, Mheshimiwa George Simbachawene ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Saada Mkuya ambaye ni Waziri wa Fedha na Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wametoa maelezo ya miswada hiyo mitano kabla haijaridhiwa na Rais Kikwete.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue pia wamehudhuria sherehe hizo ambazo vile vile zimehudhuriwa na mawaziri wa Serikali, mabalozi, wawakilishi wa taasisi zisizokuwa za Kiserikali (NGO’s) na wadau wengine wa sekta ambazo Miswada yake imeridhiwa.
Hiyo ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria hadharani. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2009 wakati Rais Kikwete aliporidhia hadharani Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha katika Uchaguzi.
Aidha, hiio ni mara ya mwisho kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria nchini kabla ya kuondoka madarakani mwanzoni mwa Novemba, 2015. Rais tayari amelivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM.
4 Agosti, 2015

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages