Breaking News

Your Ad Spot

Aug 6, 2015

PROF, LIPUMBA AACHIA NGAZI UENYEKITI WA CUF

Mwenyekiti wa Chama Cha Tanzania Civic United-CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (Pichani) amejiuzulu Uenyekiti wa Chama hicho, leo, Agosti 6, 2015.

Profesa Lipumba ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho tangu mwaka 1999, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Amesema ameamua kujiuzulu kufuatia mvutano ndani ya chama hicho ambao umefikia hatua ya kutoelewana likiwemo suala la Chama kuwemo katika Umoja wa Katiba ya Wananchi-Ukawa.

Profesa Lipumba amesema kufuatia hatua yake hiyo, atabaki kuwa mwanachama wa kawaida ndani ya Chama hicho cha upinzania ambacho ni miongoni mwa vyama vya awali kabisa vya upinzania nchini Tanzania.



Prof Ibrahim Lipumba ajiuzulu Uenyekiti Cuf,ametangaza hilo leo Aug 6.baada ya kushindwa kuelewana na uongozi wa chama hicho.



1 comment:

  1. mamuzi ya kujiuzuru ikiwa mtu halidhika na mwenendo wa mambo si mbaya. Tatizo linakuja ikiwa uamuzi huo umechochewa na jambo lisilo kuwa "takatifu". Mamuzi kama haya magumu yanatokana na kazi ya kinachoitwa *DHAMIRA ADILIFU*. Hata Mungu alimpa binadamu uwezo wa kufanya maamuzi. Biblia inatukumbusha Hawa mkewe Adamu alifanya maamuzi ya kula tunda baada ya kuahidiwa donge nono. Kwa huyu mwana siaisa siamini kuwa kulikuwepo au kumekuwepo na kuahidiwa chochote, sasa na nani kwa sababu donge nono liliahidiwa na shetani katika biblia kwa yule mke wa Adamu.

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages