Breaking News

Your Ad Spot

Aug 26, 2015

MUFT MKUU WA ZANZIBAR ASISITIZA MASHEKH NA WALIMU KUHUBIRI AMANI

Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi wakwanza kushoto akitoa maelezo juuya haki za binaadamu kwa mujibu wa Uislam wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya Haki za Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa Sheria kwa Viongozi wa Dini, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Harusi Miraji na mwisho Jina Mwinyi Waziri Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma na Sheria.
Sheikh Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar akiwafahamisha jambo washiriki wa mafunzo ya Haki za Binaadamu katika Ukumbi wa Mazsons Hotel mjini Zanzibar
Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar 26/08/2015.
Mashekhe na Walimu wa Madrasa wametakiwa kuwashajihisha Wananchi ili waepuke kujiingiza katika makundi yanayoweza kuvunja amani katika kipindi hiki cha Mchakato wa Uchaguzi Mkuu nchini.
Hayo yameelezwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi alipokuwa akifunguwa mafunzo ya Haki za Binaadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na kufanyika katika ukumbi wa Mazsons Hotel,Shangani Mjini Zanzibar.
Amesema Masheikh na Walimu hao ndio Wasimamizi wakuu katika maeneo mbalimbali ikiwemo Miskitini, Madrasani na hata ndani ya Nyumba zao kwani kufanya hivyo kutawasaidia kuepuka Uvunjifu wa Amani ni.
“Tofauti za dini, jinsia, cheo na Kabila sio njia za ukiukwaji wa Sheria ndani ya Nchi yetu bali zitumike katika kutii sharia kwa kila raia”,alisema Shekh Kaabi.


Nae Shekh Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar amewataka Walimu na Mashekhe wenzake kuwa mstari wa mbele katika kusimamia juu ya ukumbusho huo kwani kufanya hivyo ni kutekelaza majukumu yao.


Aidha amewataka Masheikhe na Walimu hao kuchukuwa juhudi za hali ya juu na kutumia maneno ya hekima, busara na unyenyekevu ili waweze kufanikiwa malengo waliyokusudia.


Hata hivyo amesema kuwa wakati wanapotoa hutuba zao ndani ya Misikiti na Madrasa ziwe ni zenye kujenga amani kwani kufanya hivyo ni kuzitii sheria zilizowekwa katika nchi yao.

Kwa upande wao Washiriki wa mafunzo hayo wamesema watayafanyia kazi bila ya kinyongo na kuyafikisha katika maeneo yao kama walivyoagizwa na Viongozi wenzao.

IMETOLEW NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages