Breaking News

Your Ad Spot

Aug 6, 2015

MSD YAWAVUTA WANANCHI KATIKA BANDA LAO MAONYESHO YA NANENANE YANAYOENDELEA MKOANI DODOMA


Wananchi wakisubiri kupata huduma katika banda la MSD kwenye Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Dodoma.

Ofisa Mdhibiti Ubora wa MSD, Betia Kaema, akitoa dawa kwa mgonjwa aliyefika katika banda la MSD kwenye maonyesho hayo.

Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dodoma, Sara Wangilisasi akitoa dawa kwa mgonjwa aliyefika kwenye banda la MSD kwenye maonyesho hayo.

Ofisa Mauzo, Juliana Mbogo na Ofisa Udhibiti Ubora, Betia Kaema wakiandaa dawa za kumpatia mgonjwa aliyefika katika banda la MSD.Na Mwandishi Wetu

Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wametakiwa kufika banda la Bohari ya Dawa (MSD), katika maonyesho ya Nanenane ili kujua kazi mbalimbali zinazofanywa na MSD hapa nchini.

Mwito huo umetolewa na Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dodoma, John Kisembi wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma kwenye maonyesho hayo ambayo kilele chake ni Agosti 8, mwaka huu.

Kisembi alisema kila mwaka MSD imekuwa ikishiriki  katika maonesho
hayo na kutoa elimu kwa wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayoihusu MSD.

Alisema mwaka huu MSD imeshiriki katika maonesho hayo ambayo yapo kikanda mkoani Dodoma ambapo wananchi na wadau mbalimbali wanaelimishwa kuhusu mambo mbalimbali ya kimafanikio yaliyofikiwa na MSD na yale yanayoweza kuongezea uwanda wao wa kibiashara hivyo kuongea mauzo yao.

Alitaja mambo yaliyozingatiwa katika maonesho hayo kuwa ni upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora kote nchini, upanuzi wa maghala hivyo kuongeza uwezo wa kuhifadhi dawa kwa wingi pamoja na usambazaji dawa na vifaa tiba kwa kutumia mfumo wa Direct Delivery (DD)

Mambo mengine ni matumizi ya mfumo mpya wa TEHAMA (Epicor 9),  Uwekaji wa nembo ya GOT katika vidonge, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara ilikutofautisha dawa za serikali na za binafsi, uanzishaji wa  maduka ya dawa ya jumla karibu na wananchi (MSD 24hours Community Outlets) , pamoja kutoa elimu, sehemu maalumu ya kutolea dawa ambapo wagonjwa wanaopatiwa vipimo katika banda la Hospitali ya Mkoa wanakuja kupatiwa dawa katika banda la MSD. 





No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages