Breaking News

Your Ad Spot

Aug 23, 2015

MAN UNITED YATOA SARE 0-0 NA NEWCASTLE

Beki wa Newcastle, Steven Taylor akinyoosha mkono juu kupinga bao la Wayne Rooney ambalo lilikataliwa leo Old Trafford kwa sababu alikuwa ameotea
TIMU ya Manchester United imepunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya England baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Newcastle United Uwanja wa Old Trafford mchana wa jana.Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney alimtungua kipa Tim Krul kuifungia timu yake kipindi cha kwanza, lakini akanyooshewa kibendera cha kuotea.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa; Romero, Darmian/Valencia dk77, Smalling, Blind, Shaw, Schneiderlin, Schweinsteiger/Carrick dk59, Mata, Januzaj/Hernandez dk67, Depay na Rooney.
Newcastle United: Krul, Coloccini, Mbemba, Taylor, Haidara, Anita, Colback, Obertan/Thauvin dk69, Wijnaldum, Perez/Tiote dk78 na Mitrovic/Cisse dk88.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages