Breaking News

Your Ad Spot

Aug 5, 2015

KAMPUNI YA ULINZI YA NIGHT SUPPOT YAANZISHA HUDUMA ZA UOKOAJI MBEYA

 Baadhi ya waandishi pamoja na viongozi wa Night Support wakiwa katika kikao
 Mazoezi yakiwa yanaendelea
 Baadhi ya watumishi
Baadhi ya Magari ya Night Support 
 
KAMPUNI ya ulinzi ya Knight Support yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam imefungua huduma mpya za uokoaji wa maisha ya binadamu na zimamoto jijini Mbeya.
 
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma hizo uliofanyika juzi katika viwanja vya Hoteli ya Mbeya, Meneja Mkuu msaidizi wa Knight Support, Ahmir Malik, alisema wamekuja Mbeya ili kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma za uokoaji kwa kuleta gari la kubebea wagonjwa na gari la zimamoto.
 
Alisema lengo la kuleta huduma hizo mkoani Mbeya ni kutokana na kupata mafanikio makubwa katika huduma ya ulinzi ambayo ilipokewa na kuitikiwa kwa wingi ikiwa ni pamoja na kampuni kujitanua kibiashara.
 
Naye Meneja mauzo wa Kampuni hiyo, Farry Desouza, alisema huduma za uokoaji zitafanywa kwa mteja kuchangia fedha kidogo ambazo zitaainishwa baadaye lakini pia kazi za kujitolea kama zitatokea kama vile kikosi cha uokoaji cha Halmashauri ya Jiji kikishindwa jambo kinaweza kuomba msaada Knight Support wakasaidia.
 
“Hatujaja kushindana naserikali bali ni kushirikiana kwani kunaweza kukatokea tatizo kubwa ambalo Fire ya Jiji ikashindwa kulimudu wakatuomba tukasaidiana vile vile hata sisi tunaweza kuzidiwa hivyo inakuwa rahisi kuomba msaada kutoka serikalini” alifafanua Meneja masoko.
 
Aliongeza kuwa watakuwepo wateja wa kudumu ambao wataweza kulipia huduma kwa Mwaka au mwezi ambao watafungiwa vifaa maalumu ambacho akibonyeza kulingana na tatizo atapata msaada wa haraka lakini kwa wateja wengine kutakuwa na huduma za simu ya mkononi itakayopokelewa masaa 24.
 
Kwa upande wake Meneja wa Kampuni hiyo Mkoa wa Mbeya, Harrison Kilai, alisema huduma zitakazotolewa zitakuwa na ubora mkubwa kutokana na vijana watakaofanya kazi hizo kupata mafunzo ya kutosha na kufaulu kutoka kwa wakufunzi ambao ni raia wa Uingereza waliobobea katika maswala ya uokoaji.
 
Alisema vijana 8 ambao ni wakazi wa Mkoa wa Mbeya wamefuzu mafunzo ya huduma za afya ambao watatoa huduma ya kwanza na kuendesha gari la wagonjwa vivyo hivyo vijana 11 wamefuzu mafunzo ya zimamoto na uokoaji.
 
Aliongeza kuwa wamelazimika kwenda sambamba na uokoaji na gari la wagonjwa kutokana na watu wengi kupata madhara wakiwa kwenye majanga hivyo wakati zimamoto likiendelea kuokoa na waliopata madhara watabebwa na kupewa msaada wa haraka kwenye gari maalum huku akikimbizwa hospitalini.

Na Mbeya

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages