Breaking News

Your Ad Spot

Aug 3, 2015

CCM KUMEKUCHA, DK. MAGUFULI KUCHUKUA FOMU YA URAIS NEC KESHO

Na Mwandishi Wetu
MGOMBEA mteule wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, kesho Jumanne, Agosti 4, 2015, atatinga Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuchukua fomu ya kuomba kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, Msafara wa Dk. Magufuli  kwenda kuchukua fomu hiyo, utaanza saa tano asubuhi ukitokea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.

Nape amesema, msafara ambao utaambatana na shamrashamra za aina yake, utapita katika Barabara za Morogoro, Bibi Titi Mohammed na Ohio kabla ya kufika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Posta House, karibu na makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Amesema, Dk. Magufuli ambaye ataambatana na Mgombea mwenza wake, Samia Suluhu, mbali na makada, wapenzi na wanachama wa CCM, atasindikizwa na viongozi mbaimbali wakiwemo, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Dk. Magufuli alichaguliwa na Mkutnao Mku wa CCM, uliofanyika Oktoba 11, 2015, mjini Dodoma, baada ya kuwashinda wagombea wenzake, Dk. Asha-Rose Migiro na Amina Salum Ally.

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages