Breaking News

Your Ad Spot

Jul 7, 2015

WATU 14 WAUAWA NA AL-SHABAAB NCHINI KENYA



Maofisa wa polisi wakiwa eneo la tukio lilipotokea shambulio lililoua watu 14 usiku wa kuamkia leo.
Takribani watu 14 wameuawa, 11 wakijeruhiwa baada ya Al-Shabaab kushambulia kijiji cha Soko Mbuzi kilichopo jirani na Mji wa Mandera nchini Kenya usiku wa kuamkia leo. Mamlaka husika huko Mandera yathibitisha.
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa shambulio lilitokea saa 7 usiku wa kuamkia leo wakati wakazi wa Kijiji cha Soko Mbuzi wakiwa wamelala.
Shambulio hilo limeelezwa kuwalenga wafanyakazi wa machimboni ambao wengi wao siyo wenyeji.

Taswira kutoka Kijiji cha Soko Mbuzi lilipotokea shambulio.

Wananchi wakiwa eneo hilo la tukio.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages