Breaking News

Your Ad Spot

Jul 1, 2015

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA SH. MIL. 65 RUFIJI

Subject: TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA SH. MIL. 65 RUFIJI To: Ahmad Michuzi , fadhili athumani , "info@dewjiblog.com" , Othman Michuzi , Cathbert Kajuna , King Jofa , Andrew Kevin Mbega , Haki Ngowi , Luke Joe , Subi Nukta , Josephat Lukaza , Jamvi la Habari Tanzania , Francis Dande , mzige , Blog za mikoani , zainul@modewjiblog.com, "uwazi@hotmail.com" , Daniel Mbega , Bashir Nkoromo , Bukoba Wadau , Bongoclan Tanzania Tv , Jestina George , Adam Mzee , verbs@rocketmail.com, Deogratius Rweyunga , Aloyson Jr , Gadiola Emanuel , Richard Mwaikenda
 Mkuu wa Wilaya ya Rufiji , Nurdin Babu akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifungua maji ya bomba mara baada ya makabidhiano ya kisima kilichochimbwa na TBL kwa gahrama ya shilingi mil. 65 katika Kijiji cha Mwaseni Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani. Makabidhiano hayo yalifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki.

 Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo, wakiwatwisha  ndoo za maji akina mama wa Kijiji cha Mwaseni, Mibuyu Saba mara baada ya kukabidhi kisima cha maji kilichochibwa na TBL kwa gharama ya shilingi mil. 65, wilayani RufijiMkoa wa Pwani. Hafla hiyo ilifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki. 

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo, wakiwatwisha  ndoo za maji akina mama wa Kijiji cha Mwaseni, Mibuyu Saba mara baada ya kukabidhi kisima cha maji kilichochibwa na TBL kwa gharama ya shilingi mil. 65, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani. Hafla hiyo ilifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki. 

Na Mwandishi wetu , Rufiji
MKUU wa wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu  amewataka wakazi wa kijiji  cha mwaseni  Mibuyu saba kulinda miradi  mbalimbali ya maendeleo hili kuweza  kupunguza tatizo la umaskini katika  eneo hilo.

Babu alisema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji hicho wakati wa makabidhiano ya Kisima kirefu cha maji safi kilicho chimbwa na Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya wakazi eneo hilo

“Kisima hiki ni sehemu ya miradi ya maendeleo ambayo imekuwa ikifadhiliwa na TBL katika jamii hivyo sio kitu cha itikadi kila mtu anapaswa kukitunza na kulinda kwa ajili ya kupunguza mzigo wa 
kwenda kufata maji mbali kwa wakina mama waishio hapa” alisema Babu.

Babu aliongeza kuwa mbali ya kuchota maji tu lazima kijiji kiweke utaratibu wa kuakikisha kuwa kila mmoja anachangia huduma kidogo hili kuweza kufanya huduma hiyo kuwa endelevu na sio ikiaribika kusubiri kutafuta mfadhili tena.

Akziungumza wakati wa kukabidhi kisima hicho Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano kutoka TBL, Stephen Kilindo alisema kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha fedha shilingi milioni 65 za kitanzania na kukabidhiwa kwa wana kijiji hao.

Alisema kuwa kisima hicho kirefu ambacho kimesambaza mabomba manne ya kutolea maji kitaweza kuhudumia watu 1700 waishio katika eneo hilo na maeneo ya jirani.

Kilindo alisema TBL kama mdau wa maendeleo na shirika ambalo uwepo wake inategemea watanzania imeamua kuchimba kisima hicho kama ni sehemu ya kurudisha kile wanacho kipata kwa wananchi hili waweze kufurahia miasha kama ilivyo katika nchi zingine duniani.

“Tanzania kilamahala kuna maji kinachohitajika ni uwezeshaji hivyo sisi kama TBL tumeliona hilo ndio maana tumeamua kujenga visima kila mahali palipo kuwa na mahitaji ya maji hapa nchini” alisema Kilindo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mwaseni Mibuyu Saba, Hasan Abdallah alishukuru  TBL kwa msaada huo mkubwa katika kijiji chake kwa kusema kuwa wameweza kutatu changamoto kubwa katika eneo ambayo inaweza kuwa chachu ya maendeleo mingine yote.\

Alisema kuna mashirika mengi sna lakini TBL kwa moyo wao wameweza kuona tatizo la mwaseni na kulibeba kama lao hivyo awana neon zaidi ya shukrani katika kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages