Waziri wa Maliasili na Utalii.
Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa na Balozi wa China nchini, Lu Youqing
wakizindua magari maalumu 50 yatakayotumika katika vita dhidi ya
Ujangili.
Haya ni baadhi ya magari maalumu
yaliyotolewa na Serikali ya China yatakayotumika katika vita dhidi ya
Ujangili. Mwingine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,
Dkt. Adelhem Meru.
…………………………………………………………………………….
Serikali ya Tanzania kupitia
Wizara ya Maliasili na Utalii imekabidhiwa msaada wa magari maalumu 50
pamoja na vifaa vya vingine 417 na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa
China ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Ujangili.
Katika makabidhiano hayo ,
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imetoa magari 50 yenye thamani ya
bilioni 2.6 yakiwemo magari yenye matairi matatu yenye uwezo ya
kutembea sehemu yoyote ya pori hata mahali pasipo na barabara ili
kuweza kuwasaidia Askari wanyamapori kukabiliana na majangili
watakaothubutu kutoroka.
Mbali ya magari hayo , China
imetoa vifaa maalumu vya kukagua makontena ili kubaini endapo
yamebeba nyara za Serikali ambapo kwa awamu hii ya kwanza vifaa hivyo
vitaanza kutumika katika Bandari ya Dares Salaam.
Akizungumza jana jijin Dares
Salaam muda mfupi mara baada ya makabidhiano hayo , Waziri wa
Maliasili na Utalii. Mhe. Lazaro Nyalandu alisema magari hayo maalumu
yatasaidia Askari wanyamapori kumudu kazi kwa kushirikiana na vyombo
vya usalama katika kuwakamata majangili popote walipo.
Amesema Serikali ya Jamhuri ya
watu wa China imeonesha njia kwa Mataifa makubwa kwa kuisaidia Tanzania
kupambana na Ujangili, ‘’ Serikali ya Tanzania haina mzaha na mtu
yeyote anayejihusisha na Ujangili, ‘’ Mhe, Nyalandu alisema.
‘’Magari haya tuliyokabidhiwa leo
yatapelekwa moja kwa moja kwenye maeneo ya kazi na kamwe hayatabaki
hapa kwa ajili ya matumizi ya maofisa,, Huu ni mpango endelevu wa
vitendea kazi kwa ajili ya Askari wanyamapori ili kuwasaidia kumudu
kazi ya kupambana na majangili’’ Mhe. Nyalandu alisema.
‘’Serikali inatoa onyo kwa
wananchi wanaowahifadhi majangili na wanaoshirikiana na majangili
ninawasihi waache mara moja’’ Mhe. Nyalandu alisisitiza
Mhe. Nyalandu amesema vita dhidi
ya Ujangili ni vita ya kidunia hivyo Tanzania imekuwa ikishirikiana
na Askari wa Kimataifa ( Interpol) pamoja na kupata msaada kutoka
kwa mataifa makubwa katika kutokomeza mtandao wa Ujangili.
Akizungumza katika makabidhiano
hayo. Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing amesema nchi
yake itaendelea kuisadia Tanzania katika vita dhidi ya Ujangili kutoka
na tatizo kubwa la ujangili lililopo licha ya jitihada kubwa
zinazofanywa na Serikali ya Tanzania.
‘’Tumeamua kuongeza nguvu katika
mapambano dhidi ya Ujangili kutokana na si Tanzania tu inayoathirika na
tatizo la Ujangili bali ni tatizo linaloathiri hata mataiafa makubwa
Makubwa ikwemo sisi’’ Balozi wa China nchini Tanzania, Bw. Lu Youqing
alisema.
Alisema wameanza kuonyesha kwa
vitendo kushirikiana na Tanzania katika vita dhidi ya Ujangili kwa kutoa
vifaa vya kisasa ambavyo vitawawezesha Askari wanyamapori kuweza
kuwasiliana kwa urahisi katika maeneo yao ya kazi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269