Breaking News

Your Ad Spot

Jul 21, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA 9 WA WAKE WA MARAIS

1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akielekea kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyetta huko Nairobi kuhudhuria mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa Nchi za Afrika unaozungumzia magonjwa ya saratani ya matiti, shingo ya kizazi na tezi dume tarehe 20.7.2015.PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI
3
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Niger Madame Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wakiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa nchi za Afrika. Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyetta (hayupo pichani) tarehe 20.7.2015.
4
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na wake wa Marais kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Kenya ukiimbwa.(VICTOR)
5
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiwa amesimama na baadhi ya wake wa Marais wa Afrika wakati wimbo wa Mataifa ya Afrika ukiimbwa. Kushoto kwa Rais Kenyatta ni Mkewe Mama Margret Kenyatta akifuatiwa na Mke wa Rais wa Namibia Mama Monica Geingos, Mama Salma Kikwete na mwisho ni Mama Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wa Niger.
6
Baadhi ya Wake wa Marais wa Nchi za Afrika wakishiriki kumvisha mkanda maalum kwa kuteuliwa kwake kuwa Balozi wa Hiari kwenye Masuala ya Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika. Wanaomvisha mkanda huo kwa niaba ya wake wa Marais ni (kutoka kushoto kwenda kulia) Princess Nikky Onyeri, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa ‘Forum of African First Ladies against Cervical, Breast and Prostate Cancer, Mama Dkt. Lalla Mahammadou wa Niger, Mama Monica Geingos wa Namibia, Mama Mary Ayen Mayardit wa Sudan Kusini. Mama Salma Kikwete na Mwisho ni Mama Mathato Mosisili wa Lesotho.
2
Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wanaoshiriki kwenye mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa Afrika wakifuatilia kwa makini sherehe za ufunguzi.
7
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Princess Nikky Onyeri, Mwanzilishi wa Forum of African First Ladies Against Cervical, Breast and Prostate cancer mara baada ya viongozi hao kutembelea Hospitali ya HH Aga Khan jijini Nairobi tarehe 20.7.2015.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages