Breaking News

Your Ad Spot

May 22, 2015

TANZANIA: HAKUNA MAENDELEO BILA NISHATI YA UHAKIKA



Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga ( Mb), akizungumzia namna  Tanzania  inavyotekeleza  Mkakati wa Nishati Endelevu kwa Wote  (SE4All) wakati wa  Mkutano wa siku mbili wa Mawaziri wa  Sekta ya Nishani,  uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, jana, Alhamisi.
Na MwandishiMaalum, New York
Tanzania  inaamini kwamba,   utekelezaji wa mipango na malengo mbalimbali ya maendeleo hayataweza kupatika au kufikiwa kwa haraka pasipo na uwepo wa nishati endelevu kwa wote.

Ni kutokana  na kulitambua hilo,  Tanzania  imejikita kikamilifu katika kukuza uwezeshaji wa matumizi ya teknolojia za kisasa na mbinu za kuongeza upatikanaji wa huduma za kisasa za nishati ikiwa ni pamoja na kuongeza maradufu kiwango cha uboreshaji na ufanisi wa nishati mbadala ili kuchagiza maendeleo.

Hayo yameelezwa siku jana Alhamisi,  na Naibu  Waziri wa Nishatina Madini, Mhe. Charles Kitwanga ( Mb), wakati wakizungumza katika siku ya pili ya majadiliano ya mawaziri wanaohusika na sekta ya nishati ambapo kila waziri aliyehudhuria mkutanohuo alipata fursa ya kuelezea na kutoa ahadi ya namna inavyotekeleza mkakati wa nishati endelevu wa wote (SE4All).

Mhe. Kitwanga naujumbe wake unaowashirikisha wataalamum balimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini akiwamo Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ngosi Mwihava wameshiriki kikamilifuka katika mkutano huu ulioitishwa na Katibu Mkuu waUmoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ambapo tangu ulipoanza mapema wiki hii, washiriki wamekuwa wakijadili mada mbalimbali zinazohusiana na masuala ya nishati, uwekezaji na mchango  wake katika eneo zima la utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

“ Tanzania inaamini kwamba hakuna ajenda za maendeleo zinazoweza kufikiwa kwa ukamilifu pasipo uwepo wanishati ya uhakika” akasemaNaibu Waziri

Nakuongeza kuwa, mkakati wa nishati endelevu kwa wote ni nyezo muhimu katika kurahisisha ukusanyaji na uwekezaji wa raslimali inayohitajika ili kufika malengo ya kitaifa ya nishati endelevu kwa wote kufikia mwaka 2034 kama inavyoainishwa katika mkakati huo.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri, Charles Kitwanga, Tanzania ilipitisha mkakati wa SE4All  mwaka 2012 na kufuatiwa na  mchakato wa kufanya tathmini  ili kubaini mapungufu ambayo yalipelekea kutoa  taarifa ya tathmini mwaka 2013

Baada ya tathmini hiyo ilifuatia  misaada kutoka  SE4All kwaajili ya Afrika iliyosaidia kuandaa rasimu ya Ripoti na  nchi ( Country Action Agenda)  kwa ufadhili wa Banki ya   Maendeleo  ya Afrika, (AfDB) na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ( UNDP).

Kwa mujibu wa Mhe. Kitwanga,  taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa  udhibitisho mwezi Agosti, 2015.

Aidha  maandalizi ya Mpango wa Uwezeshaji   umeanza na utalenga katika kuangalia mahitaji ya  haraka ili kuwezesha  mpango huo kuanza kutekelezwa.

Mkutano  kuhusu  Nishati Endelevu kwa wote  (SE4All) umefungwa   jana ( Alhamis).
 Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini ambao wamefuatana na  Naibu  Waziri  katika mkutano huu muhimu  uliojadili kwa kina  nafasi na umuhimu wa nishati endelevu kwa  wote  katika kusukuma mbele malengo ya maendeleo endelevu , ukuaji wa uchumi, maendeleo ya jamii na utunzaji  wa mazingira.



 Kitwanga akiteta jambo na  Mwakilishi wa  Bank ya Maendeleo  kwaajili ya Afrika  AfDB muda mfupi  mara baada ya   Naibu    Waziri kuzungumza ,  mkutano huu wa SE4All,  pamoja na  Mawaziri wa sekta husika umewashirikisha pia wadau mbalimbali wakiwamo wakuu wa  vyombo   vya fedha kama  vile Bank ya Dunia,  AfDB na wataalamu wengine wakiwamo pia wanamziki  maarufu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakichagiza na kuwekeza katika  nishati endelevu.
 .Kaimu Katibu Mkuu,  Bw. Ngosi Mwihava akiwasilisha  Action Agenda of Tanzania  kuhusu SE4All  katika moja ya mikutano  iliyofanyika hapa jijini  New York.
 Kaimu  Katibu Mkuu,  Bw. Ngosi  Mwihava akiwa  na wataalamu wake na wataalamu washauri  wakibadilishana mawazo kuhusu Action Plan of  Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages