Breaking News

Your Ad Spot

May 7, 2015

MAFURIKO KATIKA PICHA JIJI LA DAR ES SALAAM

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakivushwa kwenye mafuriko kwa kulipia sh. 2,000 maeneo ya Jangwani Dar es Salaam leo. Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani ilifungwa kwa muda baada ya mafuriko hayo kufunika daraja. (PICHA ZOTE KWA HISANI YA RICHARD MWAIKENDA NA KHAMISI MUSSA )
Kijana ambaye jina lake halikupatikana mara moja akimbeba msichana na kumvusha kwenye mafuriko kwa malipo ya Sh. 2,000 eneo la Jangwani Dar es Salaam leo.

Lori lililokuwa limebeba kokoto likiwa limesombwa na maji ya mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili jijini Dar es Salaam na kutumbukia kwenye Mto Msimbazi, karibu na daraja la Kinyerezi jijini leo.

Wananchi wa Bonde la Mkwajuni Barabara ya Kawawa wakiwa wamehifadhiwa jirani na nyumba ya Mjumbe Sofia Philipo baada ya nyumba zao kujaa maji leo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Nyumba zilizopo Bonde la Jangwani karibu na Klabu ya Yanga, zikiwa zimezingirwa na maji ya mvua iliyonyesha leo na kusababisha mafuruko. 
Nyumba zilizopo Bonde la Jangwani karibu na Klabu ya Yanga, zikiwa zimezingirwa na maji ya mvua iliyonyesha leo na kusababisha mafuruko. 
Kijana akiwa amebeba baiskeli yake kwa ajili ya kujitayarisha kuvuka maji kwenye bonde la Msimbazi, Barabara ya kuelekea Magomeni na Ubungo jijini Dar es Salaam.

Juu na chini: Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakivushwa kwenye mafuriko kwa kila mmoja kulipia sh. 2,000 maeneo ya Jangwani Dar es Salaam leo. Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani ilifungwa kwa muda baada ya mafuriko hayo kufunika daraja. 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages