.

BALOZI MULA MULA AAGA RASMI WATANZANIA WAISHIO MAREKANI

Jul 28, 2015

Na Mwandishi  Maalum
Katibu Mkuu, Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,   Balozi Liberata Mulamula (Pichani), amewaaga watanzania waishio nchini  Marekani,  kwa kuwataka kujivunia utanzania wao na kutoionea aibu lugha yao ya taifa,   Kiswahili.

Mwishoni mwa wiki,   Ubalozi wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania nchini Marekani,  uliandaa hafla ya aina yake  ya  kumpongeza, kumshukuru na kumuaga  Balozi Liberata  Mulamula ambaye sasa ni  Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Hafla hiyo iliyowajumuisha  watanzania wa kada mbalimbali wakiwamo maafisa na  wafanyakazi wa Uwakilishi wa Kudumu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakiongozwa na   Balozi  Ramadhan  Mwinyi,  ilipambazwa kwa nasaha mbalimbali na salamu za kumtakia kheri Balozi Mulamula katika  jukumu lake jipya.


Pamoja na  kusikiliza salamu kutoka kwa wawakilishi  wa makundi ya  kijamii,  na  kupokea zawadi,   Katibu Mkuu, Balozi Mulamula naye alipata fursa ya  kuzungumza mawili  matatu.


Katika  salamu zake  kwa watanzania  waliojumuika katika makazi yake.  Moja ya mambo muhimu  aliyoyazungumza ni pamoja na kuwaasa  watanzania waishio nchini   Marekani, kujivunia utanzania wao,  umoja wao na kubwa zaidi kutoona aibu kuizungumza na kuiendeleza lugha ya taifa Kiswahili.


“Niwaombeni  jambo moja,  msione aibu kuzungumza lugha yetu, lugha yenu ya Kiswahili,  miaka kadhaa iliyopita  watanzania waughaibuni walikuwa hawazungumzi  Kiswahili , waliogopa kujitambulisha kwa lugha yao,  lakini sasa hali imebadirika sana,  unakutana na watanzania kila kona wanazungumza Kiswahili   hili ni jambo la kujivunia sana na ninawaomba   tuendeleze utamaduni huu wa kuzungumza Kiswahili, kuwa ugenini hakumaainishi  uachane na  lugha yako” akasisitiza Balozi Mulamula na kushangiliwa na watanzania.


Katika  kutilia mkazo  wa lugha ya  Kiswahili,   Balozi  Mulamula aliwataka wana DMV kuendelea na darasa la kuwafundisha watoto  lugha hiyo ya Kiswahili na  maeneo mengine kuiga mfano huo.


Jambo  jingine ambalo Balozi  alililowasisitizia watanzania  hao ni kuhusu upendo, mshikamano, kuheshimiana, kusaidia na kutobaguana kwa misingi ya dini, kabila,  eneo  ambalo mtu  anatoka au kwa misingi ya itikadi za kisiasa.


“ Ninaondoka  baada ya miaka miwili ya kuwa   Balozi wenu,  na katika miaka hii miwili nimejifunza mengi sana kutoka kwenu, mmeshirikiana nami  na Ubalozi katika mambo mengi yakiwamo ya kuchangia maendeleo yenu wenyewe na maendeleo ya watanzania wenzenu endeleeni na moyo huu”.


Kaongeza “nitakuwa nanyi na kama  mjuavyo  tunakitengo kizima kinachoshughulia masuala ya diaspora, na kama ningekuwa mwanasiasa basi  nyie wanadiaspora mngekuwa  mtaji wangu,  jimbo langu”. akabainisha na kuamsha tena   vifijo kutoka kwa wana-diaspora hao.


Katika hatua nyingine,   Katibu Mkuu, Balozi Mulamula amewahimiza  watanzania walioko nje, kumchangamkia   hasa kwa wale wenyekutaka kujaza fomu za maombi ya pasi zao za kusafiria ambazo zimekwisha muda.

RAIS KIKWETE AFANYA ZIARA YA KISERIKALI AUSTRALIA, ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA VITA NA KUZUNGUMZA NA JUMUIA YA WATANZANIA

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kijeshi wa Fairbairn mjini Canberra katika siku ya mwanzo ya ziara yake Rasmi ya siku nne ya Kiserikali nchini Australia 

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembezwa katika jumba la Makumbusho ya Taifa ya vita  - Australian War Memorial - mjini Canberra zilikohifadhiwa  kumbukumbu mbalimbali ambayo zinazoonesha jinsi Australia ilishiriki kwenye vita mbalimbali  katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australia
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua na kutoa heshima katika kaburi la askari wa Australia wakati alipotembelea jumba la Makumbusho ya Taifa ya vita - Australian War Memorial - mjini Canberra zilikohifadhiwa kumbukumbu mbalimbali ambayo zinazoonesha jinsi Australia ilishiriki kwenye vita mbalimbali  katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australia
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na \Watanzania waishio Australia alipokutana nao na kuongea nao katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australia.

CATHERINE MAGIGE: TUMUUNGE MKONO MAGUFULI CHAGUO HALALI LA CCM

SAM_4396Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT) Catherine Magige Mkoa wa Arusha akizungumza jana katika mkutano wa wagombea Ubunge 12 kupitia chama cha mapinduzi waliofanya ziara ya kujinadi kwa wananchama pamoja na wananchi kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho jana katika mtaa wa kati(CCM Mkoa),ambapo hivi karibuni Catherine aliibuka ushindi wa kishindo kwa kura 409 kati ya kura 560 huku anayemfwatia akipata kura 248.
SAM_4403Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT) Catherine Magige Mkoa wa Arusha akisalimiana na wanachama wa chama hicho jana jijini Arusha,Aliwatoa rai kwa wananchi na wananchama wa chama cha mapinduzi kumuunga mkono mgombea Urais Dk. John Pombe Magufuli kwani ndio chaguo la CCM,huku pia akisisitiza wanaccm kuchagua kiongozi kwanzia ngazi ya udiwani,ubunge anayekubalika ndani ya CCMna nje ya CCM
SAM_4391Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau ambaye pia ni mratibu wa Mkoa akiteta jambo na Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT) Catherine Magige Mkoa wa Arusha jana katika mtaa wa kati (CCM Mkoa) wakati wa ziara ya watia nia wa chama cha mapinduzi wakijitambulisha na kujinadi kwa wanachama kuomba ridhaa ya kupitishwa na chama hicho katika nafasi ya Ubunge
SAM_4404Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT) Catherine Magige Mkoa wa Arusha akifurahia jambo na mwenyekiti wa wilaya ya Arusha katika ofisi za chama cha mapinduzi jijini Arusha jana wakati watia nia ubunge 12 kupitia chama hicho walipata nafasi ya kujinadi kwa wananchi na wanachama wa chama hicho
SAM_4289Mbunge viti maalum kundi la wanawake (UWT) Catherine Magige Mkoa wa Arusha akizungumza na waandishi wa habari siku alipotangazwa kuwa mshindi.
(Picha na Pamela Mollel)

MANCHESTER UNITED YAITANDIKA BARCELONA BAO 3 -1

Jul 26, 2015

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Barca waliweza kuonesha kumiliki mpira kwani waliweza kupiga pass 314 kwa 198 huku zikiwa zenye asilimia 90.8 dhidi ya zile 80.8 za Manchester United.
Manchester United Usiku wa Kuamkia jumapili ya tarehe 26/7/2015 waliweza kuandika historia katika Mchezo wa soka kwa kucheza Mechi na Magwiji wa soka kutoka Hispania timu ya Barcelona na Hadi kupyenga cha Mwisho ni Machester United iliyoibuka kidedea kwa Ushindi mnono kabisa wa Mabao 3 - 1 dhidi ya Barcelona.
Ni Manchester United ambao walikuwa wakwanza kuandika bao la Kwanza mnamo dakika ya 8 ya mchezo huo kupitia kwa Mchezaji Wayne Rooney ambaye alifunga Goli hilo baada ya Mpira wa Kona kupigwa na Ashley Young na Kumkuta yeye na kupiga Kichwa safi kabisa na kumuacha Mlinda mlango wa Barcelona Ter Stegen akishindwa kuokoa Mchomo huo.
HADI MAPUMZIKA MATOKEO YALIKUA Manchester United 1 - Barcelona 0

Mnamo dakika ya 60 ya Kipindi cha pili Suarez aliweza kupachika bao na kuanza kushangilia lakini bao hilo liliweza kubatilishwa na Mshika kibendela ambae alionyesha kuwa alikuwa amekwisha Jenga kibanda kabla ya Kufunga bao hilo.
Wakati huo huo Kocha wa Manchester United aliweza kufanya Mabadiliko katika kikosi chake kwa kuwatoa wachezaji 11 na mabadiliko hayo yaliweza kuleta matunda kwani dakika nne baadae Lingard aliweza kuiandikia timu yake Bao la Pili katika mchezo huo.
Mnamo dakika ya 67 Adnan Januzaj angeweza kufunga goli la tatu lakini alipaisha mpira baada ya kupiga shuti lililokosa macho na kutoka nje.
Barcelona waliwezakufanya mabadiliko kwa Sandro Ramírez kuchukua nafasi ya Pedro, Gerard Gumbau kwa Andrés Iniesta, Alen Halilovic kwa Sergio Busquets, Marc Bartra kwa Gerard Piqué na Munir El Haddadi akichukua nafasi ya Luis Suárez.
Wakati huo kikosi cha United kilikuwa ni Johnstone, Valencia, Smalling, McNair, Blackett, Lingard, Fellaini, Herrera, Wilson, Pereira, Januzaj

Rafinha aliweza kuiandikia bao pekee kwa upande wa Barcelona mnamo dakika ya 89. Lakini goli hilo halikuweza kudumu kwani dakika moja baadae Adnan Januzaj aliweza kuifungia Manchester United Goli la 3 na la ushindi katika Mechi hiyo.

Huu utakuwa ni Ushindi wa Mechi tatu mfululilo kwa Manchester United.

VIKOSI: United XI: De Gea, Darmian, Jones, Blind, Shaw, Carrick, Schneiderlin, Mata, Young, Memphis, RooneyStarting XI: Ter Stegen, Piqué, Sergio, Pedro, Iniesta, Suárez, Rafinha, Alba, S.Roberto, Adriano, Vermaelen

MTOTO MWENYE KIPAJI CHA AJABU KUTOKA MAREKANI ATUA NCHINI LEO, KUFANYA KONGAMANO LA WATOTO NA WAZAZI KESHO JIJINI DAR ES SALAAM

Jul 25, 2015

Na Mwandishi Wetu
MTOTO  mwenye kipawa cha ajabu katika kutoa ushauri  wa kujijengea uwezo wa kujiamini  anayezidi kujipatia umaarufu mkubwa duniani,  Lonnie Hudson  maarufu kama ‘King Nahh’(Pichani), ametua  jijini Dar es Salaam , leo.

King Nahh aliambatana na baba yake mzazi , Nyeeam Hudson  ambapo wapo nchini kwa mwaliko wa  taasisi isiyo ya kiserikali ya Wisdom Partners.

Kesho mtoto huyo atafanya  kongamano kubwa  la watoto na wazazi  katika Ukumbi wa Urafiki ambapo nia na madhumuni ni kuamsha hisia za  watu ambao wamekata  tamaa katika masuala mbalimbali na kukosa kujiamini katika maamuzi.

“Najisikia furaha kuja Tanzani. Ninaamini nina jukumu kubwa la kufanya hapa. Hususani  kwa watoto ambao bado hawaamini kuwa wanaweza kubadili hisia zao, kujiamini na  kushiriki katika masuala mazima ya maendeleo,” alisema.

King Nahh aliongeza kwamba, hisia za watu wengi hivi sasa zimelemaa kutokana na kuishia kulaumu  matatizo na vikwazo bila kutafuta suluhu ya matatizo yao.

“Kila mtu analaumu. Wa kwanza atalaumu, wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano mpaka wa sita. Wote wanaishia kulaumu jambo moja. Wengine wanaamini kuwa hawezi kitu. Ila ukweli ni kwamba pale unapokuwa huwezi kitu kuna kitu unaweza kufanya. Jamii ibadilike. Iache kulaumu,”alisema mtoto huyo na kushangaza watu waliokwenda kumlaki.

Mkurugenzi wa taasisi ya Wisdom Partners, Cynthia Henjewelle, alisema kuwa dhamira kubwa ya kumleta mtoto huyo nchini ni kusaidia kubadili hisia za jamii hasa watoto ili waweze kujiona kuwa sehemu ya jamii.

“King Nahh ni miongoni mwa watoto wanaosifika hivi sasa duniani kutokana na  kipawa  alichonacho. Wazazi wawalete watoto kesho  Urafiki,  ili waweze kubadilishana mawazo. Pia wazazi wanakaribishwa kumsikiliza mtoto huyu kuanzia saa tano asubuhi,”alieleza Henjewele.
HABARI KATIKA PICHA
King Nahh akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo

 Akikabidhiwa shada la mauwa uwanjani hapo
King Nahh akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kuwasili uwanjani hapo
 Meneja wa King Nahh akisisitiza jambo kwa wanahabari

 King Nahh akicheza ngoma ya utamaduni
 King Nahh akizungumza na wananchi katika viunga vya uwanja wa ndege
 Akiwa amepozi na wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo

 Akisaini kitabu cha wageni katika Supermarket ya Uchumi
 Akimlisha keki mmoja kati ya wafanyakazi wa Uchumi Supermarket
 Akilishwa keki na msanii nyota wa filamu, Iluminata Alfonce 'Dotnata'
 Akikabidhiwa 'token' na Meneja wa Uchumi Supermarket kwa ajili ya kununulia bidhaa katika kipindi atakachokuwa nchi, pembeni yake ni mratibu wa kongamano Cynthia Henjewelle
 Akitaniana na wafanyakazi wa Uchumi Supermarket
 Akijichagulia bidhaa

DR. MAGUFULI AREJEA DAR

 Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mji wa Chalinze (hawapo pichani) alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodomaakitokea Mkoani  Dodoma. 
PICHA NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP
 Wakanazi wa Bagamoyo wakimsikiliza Dkt Magufuli wakati alipokuwa akijitambulisha kwao
 Mkazi wa Bagamoyo akifurahia jambo
 Wananchi wakimshangilia Dkt Magufuli (hayupo pichani) alipokuwa akijitambulisha kwao hapo mjani mjini Bagamoyo

  Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akiwasalimia Wananchi wa Chalinze na kumkaribisha Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru Wananchi wa Chalinze (hawapo pichani) pamoja na kujitambulisha kwao alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
 Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akiwasalimia Wananchi wa Chalinze na kumkaribisha Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru Wananchi wa Chalinze (hawapo pichani) pamoja na kujitambulisha kwao alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
 Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mji wa Chalinze (hawapo pichani) alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodomaakitokea Mkoani  Dodoma.
 Wananchi wa Chalinze wakiwa wamelizunguka gari la Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Kiwangwa  alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
  Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimshangilia kwa mayowe Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Kiwangwa alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.

 Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimsikiliza Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Chalinze alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma. 
  Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo na Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli mjini Bagamoyo,aliposimama mjini hapo kujitambulisha na kuwashukuru kwa kujitokeza kwao kwa wingi kumpokea,alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
   Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete pamoja na  Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia jambo mjini Bagamoyo,aliposimama mjini hapo kujitambulisha na kuwashukuru kwa kujitokeza kwao kwa wingi kumpokea,alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
 Wananchi wakifuatilia kwa makini meneno ya Dkt Magufuli
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Rajab Luhwavi akizungumza jambo na Mh.Ridhiwani Kikwete
 Dkt Magufuli akijitambulisha kwa wakazi wa mji wa Bagamoyo mapema jana